Wanajeshi 260 wa DRC wahukumiwa kifo kisa kuwakimbia M23

Dialogist

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2014
Posts
1,167
Reaction score
1,872
Askari 260 wa Jeshi la Ulinzi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) waliokamatwa kwa kosa la kuwakimbia wapiganaji wa Kundi la M23 na kufanya uhalifu wa kivita mashariki mwa nchi hiyo, wamehukumiwa adhabu ya kifo.

Shirika la Habari la Reuters limeripoti leo Jumatatu Machi 3, 2025 kuwa kati yao, askari 55 wa FARDC walihukumiwa mahakamani eneo la Musienene Ijumaa ya Februari 28, 2025.

Zaidi ya askari 200 walitoroka baada ya wafungwa kuvunja gereza moja wakati wa uvamizi wa M23 uliosababisha Jeshi la FARDC kurudi nyuma huko Bukavu Februari 14.

Msemaji wa Kikosi cha Jeshi la FARDC linalopigana huko mashariki mwa DRC, Luteni Kanali Mak Hazukay, amesema wanajeshi walioshtakiwa wamelivunjia jeshi hilo heshima na kufanya ukatili unaoweza kuwafanya raia kuwasaidia waasi kusonga mbele.

Mashambulizi ya M23 tangu mwishoni mwa Desemba yameonekana kuwa hatari kwa vikosi vya Serikali ya Rais Felix Tshisekedi ikilinganishwa na mashambulizi ya yaliyofanywa na waasi hao takriban mwongo mmoja uliopita.

Mzozo unaoendelea Mashariki mwa DRC unatajwa kuchochewa na athari za mauaji ya Kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 na vita vya kudhibiti maeneo yenye rasilimali kubwa za DRC hususan ni madini ya Cobalt.

Waasi hao wanatajwa kuungwa mkono na Serikali ya Rwanda kulingana na wataalamu wa Umoja wa Mataifa japo Serikali ya Rais Paul Kagame inakanusha vikali madai ya kuwafadhili waasi hao.

Utetezi wao mahakamani
Mwanajeshi mmoja, Siko Mongombo Brice, ameiambia Reuters kwamba, alipoteza mawasiliano na wenzake baada ya saa kadhaa za mapigano huko Kivu Kaskazini.

Alikamatwa katika Kijiji cha Kitsumbiro na kushtakiwa kwa kuasi jeshi, shtaka ambalo amelikanusha kulitenda.

“Hii haikuwa kukimbia. Tulikuwa tunatafuta kikosi chetu,” amesema.

“Watu walituona tukiwa kwenye kijiji hiki (Kitsumbiro) hata hatujui tulifikaje hapa. Wapo waliokuwa wakiiba, lakini pia wapo watu wasio na hatia kama sisi. Mungu pekee ndiye ajuaye ukweli.”

“Tulijaribu kupambana, lakini tulishambuliwa sana kwa mabomu. Askari wa Rwanda (M23) wana silaha kali mno,” amesema kanali mmoja, akiongeza kuwa wanajeshi wa Burundi waliokuwa washirika pia walikimbia siyo wao peke yao kama inavyodaiwa.

“Tunakosolewa, lakini tunateseka kama raia wengine,” amesema kanali mmoja ambaye wanajeshi wake wamepigana katika jimbo la Kivu Kusini.

Katika kesi zilizofanyika Musienene wiki iliyopita na katika mji mkuu wa Kivu Kisini wa Bukavu, mapema Februari, waendesha mashtaka wa kijeshi waliwasilisha mashtaka kama vile wizi, uporaji, unyang’anyi na kupoteza silaha za kivita.

Wengi wa washtakiwa walikubali kuwa baadhi ya wanajeshi walihusika katika uhalifu huo, lakini walikana kujihusisha, wakisisitiza walikuwa wametenganishwa na vikosi vyao.

Usiku mmoja kabla ya waasi kuteka Mji wa Goma, mji mkubwa zaidi mashariki mwa DRC makamanda wa jeshi na mamlaka za mkoa walikimbia kwa boti kwenye Ziwa Kivu kuelekea Bukavu bila kuwaarifu wanajeshi wao, kulingana na kumbukumbu ya Umoja wa Mataifa (UN).

Matendo kama hayo kutoka kwa viongozi wa jeshi yalidaiwa kuwapunguza zaidi morali askari wa chini yao ambao tayari walikuwa wameathiriwa na mishahara midogo ya takriban Dola 100 za Marekani (Sh240,000) kwa mwezi.

Hii ni licha ya ukweli kwamba, matumizi ya kijeshi yameongezeka sana chini ya Tshisekedi, yakiongezeka zaidi ya mara mbili mnamo 2023 hadi Dola 794 milioni, kulingana na takwimu za kifedha zilizokusanywa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI).

Machafuko ya wiki zilizopita yamezidisha kuzorotesha utekelezwaji wa amri za kijeshi kwa askari wa jeshi la nchi hiyo huku ukatili dhidi ya raia ukitajwa kuongeza kulingana na kumbukumbu ya Umoja wa Mataifa iliyotoa taarifa kuhusu hali ya mapigano nchini humo.

Ingawa Serikali ya Rais Tshisekedi imekuwa ikijigamba kwa juhudi za kuajiri wanajeshi wapya na kupata silaha mpya, maofisa wa juu wa jeshi walisema hayo hayajabadilisha hali ya wale walioko mstari wa mbele, wakieleza kuwa wanajeshi bado wanakosa mishahara ya kutosha na vifaa vya kijeshi.

‘Tunasalitiwa kutoka ndani’
Rais Tshisekedi amelaumu wakuu wa jeshi lake kwa matokeo mabaya dhidi ya wapiganaji hao wa M23, huku akiwaambia wafuasi wake kwamba jeshi limesalitiwa kutoka ndani.

Hata hivyo, wakosoaji wake wanamlaumu kwa kutegemea mno vikosi vya kikanda na mamluki huku akiwajumuisha wanamgambo ambao wamekuwa vigumu kudhibiti.

“Miongoni mwa hawa wanajeshi wapya, kulikuwa na wahuni,” amesema jenerali mmoja anayeendesha operesheni za kijeshi mashariki mwa DRC.

Ofisi ya Tshisekedi, ikijibu maswali kutoka Reuters, ilisema baadhi ya wanajeshi hawana mafunzo sahihi na wanakosa ari ya uwajibikaji na uzalendo kwa Taifa.

Ilisisitiza kuwa matatizo hayo yalikuwepo kabla ya Tshisekedi na kwamba rais anataka kufanya mambo kwa njia tofauti.

Kwa sasa, hali ya ukosefu wa nidhamu inaendelea kuchochea mapigano kati ya wanajeshi na wanamgambo waliojumuishwa huko Uvira, mji ulio kwenye mpaka wa Burundi, hali inayowatia hofu wakazi wa maeneo hayo.

Chanzo cha misaada ya kibinadamu kilisema mapigano hayo yameua watu 30 mjini Uvora na kuwajeruhi zaidi ya 100 baada ya wanamgambo kujaribu kuwanyang’anya wanajeshi waliokuwa wakikimbia.

Februari 26, mwaka huu, majenerali wa FARDC, walitangaza operesheni ya kuwasaka wanajeshi wanatuhumiwa kutoroka waasi na kufanya matendo yasiyokubalika ya kinyama katika miji iliyotwaliwa na M23 ya Goma, Bukavu na karibu mji wa Uvira nchini humo.

Screenshot_20250304_101640_Instagram.jpg

===

My Take: Hii Sio Sawa. Tshekedi ni tatizo na anaua watu wake Mwenyewe. Anazidi kupunguza nguvu kazi...
 
View attachment 3258317

===

My Take: Hii Sio Sawa. Tshekedi ni tatizo na anaua watu wake Mwenyewe. Anazidi kupunguza nguvu nazi...
Hii sasa hatari, wasipouawa na waasi wanauawa na serikali!
Tshsekedi mpumbavu sana.
 
Nilikua nahisi huyu jamaa anaonewa ila sasa imethibitika bila shaka kwamba hafai kuongoza taifa kubwa kama DRC...

Haiwezekani upo katika mzozo mkubwa wa kivita bila kua na msaada rasmi toka nje, halafu wale wale wa ndani wanaopigana kwa faida yako wewe ukiwa kwenye AC, eti unaamuru wanyongwe kisa waliishiwa silaha, chakula au mbinu za kivita na kuamua kujisalimisha kwa maadui kuokoa uhai wao...
 
Hawakujisalimisha kwa maadui, wakiwakimbia ndo wakakamatwa na wenzao ambao hata hawako vita wakawapeleka kambini wakawashtaki na sasa wanawauwa wao.
Badala ya kuwapa mafunzo vizuri na silaha warudi tena kupigana wanaamua kuwauwa.
 
Back
Top Bottom