Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Wanajeshi wa Korea Kaskazini ambao wamejiunga na vita vya Ukraine kwa niaba ya Urusi wamepata uhuru wa kutumia intaneti isiyo na vikwazo kwa mara ya kwanza na kujikuta wakitumia uhuru huo kutazama picha za ngono, kulingana na ripoti ambayo haijathibitishwa na afisa wa Pentagon.
Kwa mujibu wa mwandishi kutoka Financial Times, Gideon Rachman amenukuliwa akisema "Chanzo cha kuaminika kinaniambia kuwa wanajeshi wa Korea Kaskazini ambao wametumwa Urusi hawajawahi kupata mtandao wa intaneti usio na vikwazo.
Kwa sababu hiyo, wametumbukia katika uraibu wa kuangalia ponografia” Rachman hakutoa muktadha zaidi wa jinsi chanzo chake kimejua tabia za mtandao za wanajeshi 10,000 wa Korea Kaskazini waliotumwa na Kim Jong Un ili kuimarisha juhudi za vita za Putin.
Source: Sky News