Urusi anahusika vipi na comment yangu !?Abraham Lincoln haina mjadala imekaa miezi 9 majini ikifanya kazi, imezidisha miezi 3 ya deployment.
Nionyeshe carrier ya Urusi iliyokuwa deployed kwa siku 1 tu. Ni ipi?
Mkuu unachekesha kizazi hiki Vita inapiganwa kwa drone wewe unatetea hizo ngalawa za USA😂. Urusi mwenyewe aliona ni upuuzi kuwekeza kwenye aircraft carrier akawekeza kwenye makombora ya masafa marefu!Aircraft carrier imekaa baharini miezi 9. Wanajeshi ndio wameshindwa kukaa zaidi ya hapo, sio meli.
Wenzako wa Urusi nitajie ni lini meli yao yoyote uliwahi kaa majini mwezi mmoja tu inafanya kazi.
The last time wamejaribu kuipeleka voyage Admiral Kuznetsov ilifuka moshi ikabidi tugboats zije kuivuta, UK wakakaa chonjo ikitokea changamoto wawaokoe Warusi.
Baada ya hapo ikapelekwa shipyard ikakaa miaka zaidi ya 7 imepaki. Walipokuja kufanya testing ikazamisha floating deck.
Mpaka sasa Russian Navy haiwezi endesha carrier walau siku 1. Wala hawana mechanism ya kuibeba kutoka berth maana ilizamisha deck kubwa pekee iliyokuwa na uwezo huo.
Leo hii wewe wa kucheka Wamarekani kuwa sea sick baada ya kukaa majini miezi 9. Ikiwa ni baada ya kuzidisha miezi 3 ya deployment?
Kilichotokea hapo ni fatigue na deko la wanajeshi wa Marekani. Ambalo of course wa Urusi hawawezi kuwa nalo, maana hawana carrier ya kufanya kazi saa 24 tu achana na miezi 9.
Moja ya sifa ya Lincoln nikukaa baharini kwa miaka mingi hapa inaletewa tu msosi sababu inatumia nyuklia inaweza kukaa miaka mingi hata 20Nani alikueleza US carrier inatakiwa kukaa majini miaka 10?
Unahisi kwanini waliunda carriers nyingi kama ndio hivyo?
Ni jeshi gani duniani ambalo wanajeshi wake wanakuwa kwenye combat zone miaka 10 bila mapumziko?
Bado nasubiri unitajie carrier ya Urusi ya kukaa majini siku moja ni ipi.
Naona umeamua kuja na mipasho badala ya factKauli za kujitungia hazifichi ukosefu wa carrier kwa hilo jeshi njaa unaloshabikia.
US Navy hawajawahi tamka popote kuwa carrier inabidi ikae majini kwa miaka 10. Kama unaamini kuna jeshi duniani litapeleka combatants wakae front line miaka 10 basi achana na mijadala ya jeshi jadili tende na ngamia.