Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Wanajeshi wawili wamewaua kwa risasi watu 15 katika mashambulizi tofauti mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wahasiriwa takriban wote walikuwa raia.
Haya yanajiri baada ya watu sita kujeruhiwa wakati wanajeshi waliporusha guruneti kwenye umati wa watu walipokuwa wakijaribu kuwakamata.
Afisa mmoja katika jimbo la Kivu Kusini alisema mwanajeshi aliyekuwa mlevi kwenye boti kwenye Ziwa Tanganyika aliwaua abiria wanane wakiwemo watoto kabla ya kukamatwa.
Siku ya Jumapili mwanajeshi mwingine alimpiga risasi kanali mmoja, mlinzi wake na raia watano katika jimbo la Ituri. Muuaji huyo ambaye pia inasemekana alikuwa mlevi, alipigwa risasi na mwenzake alipokuwa akikimbia.
Kwa zaidi ya miongo miwili watu kote mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamevumilia mashambulizi ya mara kwa mara na makumi ya makundi yenye silaha.
Rais Félix Tshisekedi amesema kukomesha ghasia hizo ni kipaumbele cha kwanza kwa serikali yake.
Hali ya kuzingirwa iliwekwa kwenye majimbo mawili karibu mwaka mmoja uliopita.
Lakini ilikuwa na athari ndogo kwani waasi na wakati mwingine wanajeshi wa Kongo wasio na nidhamu wanaendelea kusababisha uharibifu.
Chanzo: BBC