WanaJF mnakumbuka hii hadithi? Sadiki na Chitemo

 
Jina la chitemo sijaliona kabisa badala yake nimeona jina jipya la chitemo.
 
Sadiki kwanini hakumpeleka studio ndugu yake??? Tungekuwa na akina harmonize wawili saivi
 
Dah nakumbuka drsa la 3 hyo tulifanya igizo nikawa sadiki

Its not over until its over...[emoji769]
 
Lipa kodi kwa maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania
 
Hizi ndizo hadithi za ujima...asante sana kesho tukumbushe chopeko na mnofu!
... hizi ngano zimetia watanzania hofu sana tena sana! No wonder watanzania ni watu wa hofu tu na kutojiamini kuanzia aliye mkubwa zaidi hadi yule mdogo wa mwisho! No confidence; watu wa hofu tu. Aina hii ya maandishi ni kupiga chini kwenye mitaala zetu na ku-introduce za ku-impart watu confidence otherwise kama taifa hatuchomoki.

In my opinion "mkaidi" Sikiri was better than "mtii" Sadiki! Ukaidi wa Sikiri ni wa kijasiri na angeweza kufanya makubwa kama asingejazwa hofu aliyokuwa anajazwa na jamii. Utii wa Sadiki alikuwa analelewa kuwa mjinga na mwelekeo wa "ndio mzee". Why chakula kinatumika kama silaha? No wonder leo watu wako tayari "kutii" japo kinafiki kwa ajili ya matumbo yao - full unafiki kila mahali kwenye siasa, vyombo vya maamuzi, n.k.

Mwamba kaamua kuzamia gari (mnakumbuka TTBS?) bahati mbaya alikosa "mawe" vinginevyo angekuwa mjini na kuachana na "ushamba" wa kijamii. Leo hii pengine angekuwa mtu mwingine kabisa wa kupigiwa mfano katika jamii.
 
Zama zile smartphone hazikuwepo. Nilijenga tabia ya kupendelea vitabu sana hasa vya hadithi. Leo hii ukinunua kitabu cha hadithi ukiweka nyumbani hakuna wa kusoma. Watoto wanataka uwape laptop yako au smartphone wacheze game la spider.
 
Hiyo ni second edition,wakongwe tunajua Sikili na Sadick
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…