WanaJF, Naomba Uenyeji

Gaston Mbilinyi

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2010
Posts
296
Reaction score
51
WanaJF Wapendwa,

Salaaam!

Nimekuwa nikitembelea 'the Home of Great Thinkers - JF' na kuwasomeni kama mgeni kwa muda sasa.

Hapa JF ugeni ni mbaya kwani unasoma na kuhabarika, pa kucheka unacheka na siku alaulah zinaongezeka, lakini hauwezi kuuliza au kuchangia chochote mpaka umekaribishwa!

Hivyo kwa ujumbe huu naomba mnipokee na kuniondolea ugeni huu ili niwe mmoja wenu hapa JF.

Natanguliza shukrani kwasababu naamini nyie hamnaga mipaka kama ya Tz na Malawi kwa atakaye kuungana na kushirikiana nanyi. Hivyo naamini kuwa mtanipokea.

G. Mbilinyi
 
Kuku mgeni hakosi kamba mguuni so karibu ila uwe mnyenyekevu kwa wenyeji wako nao watakukirimu vizuri xana.
 
Karibu sana, jaribu kupitia kanuni na sheria za JF kwa umakini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…