Blaki Womani
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 11,229
- 13,442
Jana usiku amekuja rafiki yangu ameolewa na ana watoto 2 wiki mbili zilizopita mumewe alikuja na mgeni mwanamke nyumbani bila taarifa kwa mkewe akamtambulisha ni mwanafunzi walisoma nae wakati akiwa Uholanzi. Mkewe hakuwa na lakufanya akamkaribisha mgeni na kumwandalia chumba cha kulala. Huyo dada ametokea Afrika ya Kusini anasema wakati wakisoma alipenda kutembelea Tanzania na aliomba huyo mume awe mwenyeji wake na alipofika walikwenda kutembelea mbuga za wanyama kwa muda wa siku 4 wakarudi na yule dada ameondoka amerudi kwao South Africa. Sasa yule mke anasema ana wasiwasi yule ni kimada wa mumewe amejaribu kumwuliza mumewe kuhusu huyo dada lakini mpaka sasa mumewe anasema ni rafiki amependa kutembea Tanzania
ananiomba nimpe ushauri maana yeye haamini jibu
nisaidieni wanaJF
ananiomba nimpe ushauri maana yeye haamini jibu
nisaidieni wanaJF