WanaJF niokoeni mwenzenu,mitishamba ya kutibu tatizo la tumbo

WanaJF niokoeni mwenzenu,mitishamba ya kutibu tatizo la tumbo

ufumawicha

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
504
Reaction score
209
Ni mwaka wa 18 naumwa tumbo linanikata na kuunguruma.Mara naharisha mara inakata.Hadi muhimbili nimefika.Dawa nimetumia nyingi hadi chumba changu kinaitwa minipharmacy.Kwa anayejua mitishamba anijuze please!!Kwani cha ajabu kila nikipima vipimo vinaonyesha malaria,amiba,minyoo au taifod na dawa natumia ila wapi!Nimeanza kutafuna vitunguu saumu ndiyo kidogo napata ahueni,ingawa si sana!
 
Nina dawa nzurisana ya mitishamba inayotibu na kuondoa tatzo hilo.kwa msaada zaid ntafute,0759217720.
 
Hiyo kuchanganya madawa ndio inayokudhuru!

Ngoja nikufafanulie kitu hapo:
Always mtu hupona kwa vitu viwili!
1 Imani!
2 Nguvu za dawa!

Sometimes unaweza kupona kwa dawa tu! Refer wale wagonjwa waliopoteza fahamu! = nguvu za imani hajifanyi kazi kutokana na kutojitambua!

Sometimes mtu anaweza kupona kwa imani tu endapo atatumia dawa (sahihi) na kuamini atapona! Kwa mantiki hiyo, unaweza kutumia dawa sahihi na usipone kutokana na imani yako kutokubali kwamba utapona!

Na hili huenda ndio tatizo lako!
Kwa stage uliofikia wewe ni wazi umeshaamini wewe kupona ni vigumu! Na hali hiyo itakukost sana!

May be, mwanzoni ulipotumia dawa uliamini utapona but kutokana na dawa ulizotumia kutokukubali/kushindwa kukuponesha imekujengea hali ya kutoamini dawa unazotumia!

Hali hiyo kisaikolojia inatambulika kama Anxiety disorder! Ili kutatua tatizo lako, you must confirm your faith fast na uondoe hofu iliyojijenga katika moyo na akili yako!

I hope umenielewa hapa!
Nakutakia kila la heri!
Pole sana!
 
Ni mwaka wa 18 naumwa tumbo linanikata na kuunguruma.Mara naharisha mara inakata.Hadi muhimbili nimefika.Dawa nimetumia nyingi hadi chumba changu kinaitwa minipharmacy.Kwa anayejua mitishamba anijuze please!!Kwani cha ajabu kila nikipima vipimo vinaonyesha malaria,amiba,minyoo au taifod na dawa natumia ila wapi!Nimeanza kutafuna vitunguu saumu ndiyo kidogo napata ahueni,ingawa si sana!
Pole sana kwa hayo matatizo yako ingawa hujatuambia wewe ni mke au mume?

imekuwa vizuri Hospitali wameyaona hayo maradhi yako ingelikuwa hawayaoni tungelisema umefanyiwa ( Ulozi) mambo ya kiswahili elimu

ya giza ila tunashukuru unayajuwa yale unayo umwa. Na kuhus hicho Kitunguu saumu unakitumiaje kwa hayo matatizo yako?

Ungelikuwa unakila kila siku Asubuhi unapo amka kabla ya kula kitu au kunywa kitu fanya hivi:

Nunua kitunguu swaumu.Menya chote kama vile uandaavyo kwa ajili ya kupikia.Twanga ama saga,vikishasagika changanya na maji ya

uvuguvugu kidogo kipimo cha kijiko cha chai ili vilainike.Chota msagiko wote wa vitunguu na uvimeze.

Tahadhari,jitahidi uwe na mfuko ama sehemu ya maliwatoni maana kama hauna tumbo zuri unaweza tapika.(Mara chache sana hutokea

kutapika)


Ukishakaa kama dk 15 hali yako kuto tapika itarudi kawaida.Baada ya SIKU 7 utaona hakuna tena malaria,amiba,minyoo au taifod

Pia kama una presha ya kushuka usitumie hii dawa maana huwa inashusha sana presha,labda unywe na kahawa baada ya kuinywa

dawa hii ili kuipandisha tena presha! Tumia kwa Asubuhi kwa muda wa siku 7 na kama unaona harufu ya kitunguu Saumu

inakusumbuwa baada ya kula kitunguu saumu tafuna karafuu au tafuna Tangawizi mbichi ili kuikata harufu ya kitunguu Saumu. Unaweza

kuwa unakula punje 2 asubuhi za kitunguu saumu punje 2 mchana za kitunguu saumu na punje 2 usiku kabla ya kula kitu uwe unatumia

kwa njia hiyo kwa muda wa siku 7 kisha nenda kapime hayo maradhi yako utaona umekwisha pona. Dawa ingine uwe unakunywa

Asubhi kabla ya kula au kunywa na kabla ya kwenda chooni kupiga mswaki Glasi 2 za Maji ya uvuguvugu kwenye hiyo glasi 1 tia kijiko 1 Asali

safi ya nyuki na kamulia limau 1 zima.

ukisha piga mswaki kunywa tena glasi 1 ya Maji ya uvuguvugu kisha kaa bila ya kula kitu kwa muda wa saa 1 kisha unaweza kula. Na

wakati wa mchana kunywa maji ya uvuguvugu glasi 2 kabla ya kula chakula cha mchana kisha kaa baada ya saa 1 kupita waweza kula

chakula. Na wakati wa usiku saa moja kabla ya kula hakula cha usiku kunywa tena Maji ya uvuguvug glasi 1 kisha kaa baada ya saa 1

kupita waweza kula chakula cha usiku na wakati wa kwenda kulala kunywa tena Maji ya uvuguvugu glasi 1 kisha lala dumisha hivyo kila

siku utapona na kuumwa kwako na hayo maradhi ya tumbo na mwili mzima utakuwa na Afya njema kwa sababu Maji ya uvuguvugu ni

dawa kwa kila maradhi tumia kisha uje unipe feedbck.


dokta MziziMkavu tafadhari mkuu tunaomba msaada wako huku!!!
Mkuu Majigo hujambo lakini?
 
mzizimkavu,nakushukuru sana kwa maelezo yako!Kama ulivyoniuliza mimi ni mwanamume baba wa mtoto mmoja!
 
dokta mi niko salama kabisa nashukuru mtu wangu anaendelea kutumia ile dawa
ila alkariyaat ni chungu balaa
pia ahsante kwa kuitikia wito wa ndugu yetu hapa!
 
Back
Top Bottom