Mkuu mimi si mtaalamu wa hii maneno lakini i can imagine how simple it is.
Kama watu wote wanatuma kwenye center no moja mfano 1555 inamaana msg zote zitaenda huko kwahiyo ni rahisi kujua ngapi zimetumwa, pili kila mtandao wanabei yao ya sms, mfano voda 56, tigo 40 nk na makubaliano ni kuwa kila sms itatozwa 250, na hapo pia kutakuwa na makubaliano kati ya mitandao na waandaaji, mfano ktk sms moja voda watakata 60 inayobaki inaenda kwa waandaaji. mwisho wa siku mitambo inarekodi kila kitu waandaji wataenda voda watapewa cha juu chao,na tigo hivyo hivyo na airtel.
Ambacho sina uhakika nacho ni kuwa nasikia kunakampuni nyingine ndio inamiliki hizo namba, unakwenda kwao wanakupa code no yako mfano 1555 kisha unakwenda ktk mitandao kukubaliana nao juu ya makata na malipo kisha kazi inaanza mwisho mgao unatembea according to makubaliano.
issue ya kujua nimtandao gani umetuma kiasi gani cha sms ni very simple kama ilivyo simu yako inavyoweza kuainisha.
Mitambo yao ni mikubwa inaoption nyingi za kuainisha kumbukumbu licha ya kujua mtandao gani inajua nani katuma mara ngapi tarehe na saa ngapi na zimetumwa kutokea sehemu gani ya mnara uliotumika nk.