Wanamgambo waua wanajeshi 30 Nigeria

Wanamgambo waua wanajeshi 30 Nigeria

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wanamgambo wenye msimamo mkali wameuwa wanajeshi 30 wa serekali katika mfululizo wa mapigano kaskazini mashariki mwa Nigeria toka Jumatano, kwa mujibu vyanzo vya kijeshi na raia.

Shirika la habari la Reuters linaeleza kwamba usalama kote Nigeria, umezorota katika miezi ya hivi karibuni ikijumuisha kaskazini mashariki.

Mashambulizi manne yamesababisha vifo vya wanajeshi 27, na wanamgambo wa kikosi cha raia 10, ikijumuisha mkuu wa kikosi, kwa mujibu wa chanzo cha Reuters.

Jeshi na msemaji wa wizara ya ulinzi hawakuwa tayari kujibu simu na ujumbe uliopelekwa ili kutoa ufafanuzi wa habari za mashambulizi hayo.

Kundi la Islamic State West Province (ISWAP), ambalo lina ushirikiano na kundi la Islamic State, limedai kuhusika na mashambulizi ya Ijumaa ya Monguno, kupitia shirika la habari la Amaq siku ya Jumamosi.

ISWAP limedai kuua wanajeshi 33 na kumkamata mmoja.

1615782001389.png
 
Hawa uzuri wao wana maeneo wanayoyakalia, inahitajika offensive operation ya kuwashambulia mfululizo.

Inashangaza jeshi na vifaa vyao vyote wanasumbuliwa na vikosi vya wanamgambo Tena wanajulikana maeneo walipo.
 
Awa jamaa watakua na jambo nyuma ya pazia sio bule bhana haiwezekani jeshi lishindwe kuwazibiti mgambo.
 
Hawa wanamgambo tatizo lao wanatumia raia wa kawaida kama kinga.
Sehem km hizo ni kujenga kambi za jeshi na kupeleka watu wenye roho katili sana patatulia maana ni miaka kibao wamekua wanaua watu nanserikali ipo tu.
 
Inahitajika roho ngumu sana Ku deal na hawa jamaa.

Tatizo lao hawa wavaa kobazi wakishafanya mashambulizi wanarudi ma kwao na kuwa kama raia wema kabisa na huta wajua kabisa pakitulia mnafanyiwa ambush tena mpaka mkome.

NB: Jeshi la wala rushwa kamwe haliwezi kushindana na hawa jamaa hata siku moja.
 
Nyinyi na hiyo dini yenu ndo maana mnachukiwa na mnahusishwa na ugaidi
Umeniquote Bila kunielewa mkuu.

Nimesema kuwa nia na madhumuni ya Wanamgambo hao Ni kusimamisha dola la Kiislamu.

Kuna wanaojiita herdsmen wapo maiduguri. They have the same mission Ila wanapata resistance kubwa kutoka kwa igbos... indigenous peoples of Biafra.

Kuna stori kubwa Sana behind machafuko yanayoendelea huko.

Yote hayo yanasababishwa na ukosefu wa elimu.
 
umeniquote Bila kunielewa mkuu ...

Nimesema kuwa nia na madhumuni ya Wanamgambo hao Ni kusimamisha dola la kiislamu.
Kuna wanaojiita herdsmen wapo maiduguri ... They have the same mission Ila wanapata resistance kubwa kutoka kwa igbos... indigenous peoples of Biafra.
Kuna stori kubwa Sana behind machafuko yanayoendelea huko.

Yote hayo yanasababishwa na ukosefu wa elimu.
Asante kwa kunielimisha
 
Swala hapo ni kuigawa Nigeria tu
Mkuu na wakilogwa kuigawa nigeria kisa hao wapuuzi basi watakua wameaapa nguvu sana hata kuanza vita nchi nyingine wapate sehem wafanye yao.Hao nikupeleka jeshi ua hata raia wanao kaa nao maana km ww ni raia mwema umekaa na gaidi hutoi taarifa serikalini na ww si gaid.
 
Hawa uzuri wao wana maeneo wanayoyakalia, inahitajika offensive operation ya kuwashambulia mfululizo.

Inashangaza jeshi na vifaa vyao vyote wanasumbuliwa na vikosi vya wanamgambo Tena wanajulikana maeneo walipo.
Mkuu wangu hawa mafala wana advantage moja...kuna wakati wanavaa kiraia tena kama wanawake wanajifunika yale manguo.
Hakuna vita ngumu kama kupigana na gaidi
 
Awa jamaa watakua na jambo nyuma ya pazia sio bule bhana haiwezekani jeshi lishindwe kuwazibiti mgambo
Mgambo na mwanajeshi wote ni binadamu wanaofanana na wote ni wapiganaji.....
usiwe mislead na hilo neno mgambo ukawadharau
 
umeniquote Bila kunielewa mkuu ...

Nimesema kuwa nia na madhumuni ya Wanamgambo hao Ni kusimamisha dola la kiislamu.
Kuna wanaojiita herdsmen wapo maiduguri ... They have the same mission Ila wanapata resistance kubwa kutoka kwa igbos... indigenous peoples of Biafra.
Kuna stori kubwa Sana behind machafuko yanayoendelea huko.

Yote hayo yanasababishwa na ukosefu wa elimu.
Vuguvugu la Igbo haliuwi au kuteka wanafunzi kwa Ransom, Nigeria kaskazini asilimia 90+ ni waislamu na wengi Wana elimu ya dini na hawataki kusoma elimu ya magharibi, watu Kama ni rahisi kuwa recruit na wanamgambo

Kusini mjimbo mengi ni wakristo Ila hakuna masumbulio ya ugaidi Kama kaskazini, Ila ujambazi ni mkubwa na watu kutekwa kwa Ransom in short Nigeria is a failed state
 
Back
Top Bottom