Wanamichezo 5 wa Cameroon watoweka kambini Australia kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola

Wanamichezo 5 wa Cameroon watoweka kambini Australia kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Maafisa wa timu ya Cameroon inayoshiriki michezo ya Jumuiya ya Madola inayoendelea Australia wamesema wanamichezo watano kutoka kambi yao wametoweka.

Wanyanyua vyuma watatu na mabondia wawili hawajaonekana tangu jana na kuzua tetesi kwamba wametoroka wakiwa na nia ya kutorudi Cameroon. Tukio hilo limeripotiwa kwa polisi wa Australia.

Waandalizi wa michezo ya Jumuiya ya Madola wamewataka washiriki waheshimu sheria, ikizingatiwa kwamba zaidi ya wanariadha 100 walipitisha muda wa kurudi katika visa zao katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2000 huko Sydney.



WhatsApp Image 2018-04-11 at 15.06.32.jpeg


Chanzo: DW
 
Yaani fursa hizi utafikiri "Escape to victory"

Halafu mmoja wa boxing alikuwa apigane jana
 
Back
Top Bottom