Wanamuziki watano wa Hip Hop matajiri zaidi duniani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532



Utajiri wa mwanamuziki Jay Z ulipanda kwa asilimia 30 mwaka jana na kufikisha utajiri wake hadi $810m (£626m), kwa mujibu wa jarida la Forbes. Lakini kuimarika kwa utajiri wake hakukutosha kumuondoa Sean "Diddy" Combs kutoka kwenye kilele cha wanamuziki matajiri zaidi wa Hip Hop kwa mujibu wa jarida hilo.

Diddy anaongoza akiwa na utajiri wa jumla ya $820m (£633m).
Forbes walisema utajiri wake ulioimarishwa na mikataba ya kibiashara ambayo alitia saini na Diageo kwa ajili ya Ciroc vodka na mavazi yake ya Sean John.



Lakini rapa na produsa Jay Z alipanda hadi nafasi ya pili sana kutokana na uwekezaji wake wa $200m (£155m) katika kampuni ya kuuza muziki mtandaoni ya Tidal.
Pia, ana mvinyo kwa jina Armand de Brignac, na anamiliki pia Roc Nation



Mwaka uliopita, utajiri wa Diddy ulikuwa $750m (£579m) na wa Jay Z $610m (£471m).
Forbes waliandaa orodha yao wakizingatia mapato ya miaka ya nyuma pamoja na stakabadhi za kifedha, thamani ya mali inayomilikiwa na wanamuziki hao na pia kwa kuzungumza na wachanganuzi, mawakili, mameneja na wataalamu wengine katika tasnia ya muziki.



Rapa wa zamani wa NWA Dr Dre kwa sasa ana utajiri wa $740m (£571m) baada ya kuuza Beats kwa Apple mwaka 2014 kwa $3bn (£2.3bn), lakini amepitwa na Jay Z kwa mara ya kwanza.
Baada ya kuuza Beats, alinunua jumba kubwa la kifahari Los Angeles la ukubwa wa futi 14,000 mraba kwa $40m (£31m).
Rapa ambaye pia ni mmiliki mwenza wa Cash Money Records Bryan "Birdman" Williams ana utajiri wa $110m (£85m).



Lebo yake ambayo huimiliki na ndugu yake Ronald (Slim), ina wanamuziki nyota duniani kama vile Drake, Nicki Minaj na Lil Wayne.
Drake utajiri wake unakadiriwa kuwa $90m (£70m).



Aliingia kwenye orodha ya wanahip-hop watano matajiri zaidi duniani na anadaiwa kujizolea jumla ya $1m (£773,000) kila usiku wakati wa ziara yake ya muziki duniani mwaka jana.
Pamoja na kulipwa kutokana an mauzo ya muziki wake, pia ana mikataba ya kibiashara na Apple, Nike na Sprite.



mwanazuoni online
 
Hivi Dre baada ya kuuza beats by Dre kwa Apple huo utajiri wake umepukutikia wapi? Alitakiwa awe namba moja kwenye List
 
Namkubali sana mnyamwezi wangu Diddy, muziki aliuacha kitambo lakini kumaintain jina lake kwenye biashara hawamuwezi, namtabiria Dre baada ya miaka mitatu pesa yake kupukutika maana biashara hawezi kilichombeba ni ile neema ya apple tu. Kuhusu Drake naona kama yuko slow, kwa jinsi nnavyosikia anavunja marekodi ya mauzo nilitegemea atakuwa anawakaribia kina Jigga kumbe bado ana safari ndefu sana
 
Nilimsikia Diamond akisema yeye ni mwanamziki Tajiri wakati anahojiwa na Clouds mbona simuoni hapo kwenye list? Au Mwanamziki Tajiri wa MADALE?
 
Kwani kabla ya deal na Apple Dre alikuwa hana hela?
 
Diddy ajipange jigga anakamata usukani muda c mrefu drake asipomaintain atadondoka birdman namkubali hawezi shuka,
 
Wapo wapi wagonga ngoma kali za kileo kina Rozayyyyyy,Meek Mill,Future,Young thug,nk
 
Hivi Dre baada ya kuuza beats by Dre kwa Apple huo utajiri wake umepukutikia wapi? Alitakiwa awe namba moja kwenye List
Mkuu, "Beats by Dre" haikuwa ya Dre peke yake. Ilikuwa ni joint venture, kuna watu wengine pia waliwekeza humo. Ilipouzwa kila mwekezaji alipewa pasu kutokana na hisa zake, sio kwamba Dre alipewa $3Bn zote. Halafu Uncle Sam naye lazima alichukua zake humo humo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…