Wananch wamelala kuhusu kujilinda wenyewe – Mwema

omujubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2011
Posts
4,326
Reaction score
2,506
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema amesema hadi sasa asilimia 89 ya Watanzania wanaamini jukumu la kulinda maisha na mali zao linahusu polisi na Serikali, kitu ambacho siyo sawa.

Akipokea zawadi kutoka Benki ya Exim kwa ajili ya askari watano kutokana na utendaji kazi bora, Mwema alisema takwimu zilizopo zinaonyesha mwamko wa Watanzania kuelewa na kushirikiana kulinda mali zao, bado uko chini kwani ni asilimia 11 ndiyo imeamka na kuelewa.

Je, kwa mwendo huu tutafika huko tunakokwenda!??

Source: Mwananchi 16 Agosti 2012
 
Kwani polisi wameajiriwa kwa kazi gani au wanafikiri kuzuia maandamano ndio kazi yao.Wakati madaktari wanalalamika juu ya ukosefu wa nyumba wao wamejengewa na mifuko ya wafanyakazi ingawa wafanyakazi wakigoma wao ndio wa kwanza kwenda kuingilia kati.tatizo la uteuzi wa kujuana lakini kuna tofauti kubwa ya utendaji wa wakuu wawili wa polisi wawili waliopita na wakuu wa polisi waliokuwepo kabla ya hapo.Hao wawili wamekuwa karibu zaidi na wafanyabiashara kama Mahita alivyoenda kufungua duka la kajumulo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…