Nadhani niliweka uzi jana kama si juzi kuhusu kiupepo hiki cha wananchi kuhojiwa wakisifia OR TAMISEMI kusimamia vizuri mchakato wa wagombea kuchukua fomu na mpaka tamko la muda kuongezwa.
Yaani walitengeneza tatizo, wakasubiri lifukute, halafu wakalitatua, sasa wanaanza kujisia kwa kufanya vizuri. Kwenye picha hii JamiiForums na JF Toons wamecheza kama pele;
Ujinga ni kwamba mnawapa watu wa kusifia ambao hata script wanashindwa kumeza! mnabaki kuaibika, ni fezea!
Haya tuendelea kuangalia maigizo, kule ndani wanatifuana basi ni vurugu mechi!