Pre GE2025 Wananchi Handeni - Tanga waishukuru Serikali kwa kutatua kero ya upatikanaji wa huduma ya maji

Pre GE2025 Wananchi Handeni - Tanga waishukuru Serikali kwa kutatua kero ya upatikanaji wa huduma ya maji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wakazi wa Bongi, wilayani Handeni mkoani Tanga, ambao walikumbwa na changamoto ya uhaba wa maji na kulazimika kutembea umbali wa kilomita 3 hadi 4 kutafuta huduma hiyo, sasa wanapata maji karibu na makazi yao kufuatia juhudi za serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia, kama kiongozi wa nchi ameendelea kusimamia jitihada za kuhakikisha wanawake wanapata huduma ya maji karibu na maeneo yao ili kuwaondolea mzigo wa kutembea umbali mrefu.

Hatua hii imewezesha wakazi wa Bongi kupata maji safi na salama, hali inayoboresha afya zao, kuongeza muda wa kushiriki katika shughuli za kiuchumi na kijamii, na kupunguza hatari wanazokabiliana nazo wakati wa kutafuta maji.

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Handeni wakazi wake akili zao zinafanana.wakazi wa handen hadi leo hawajui maji ya bomba.watoto wakiona bomba wanashangaa.ni sehemu pekee mwenyekiti wa ccm ana mamlaka kupita hata serikali kuu.
 
Wakazi wa Bongi, wilayani Handeni mkoani Tanga, ambao walikumbwa na changamoto ya uhaba wa maji na kulazimika kutembea umbali wa kilomita 3 hadi 4 kutafuta huduma hiyo, sasa wanapata maji karibu na makazi yao kufuatia juhudi za serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia, kama kiongozi wa nchi ameendelea kusimamia jitihada za kuhakikisha wanawake wanapata huduma ya maji karibu na maeneo yao ili kuwaondolea mzigo wa kutembea umbali mrefu. Hatua hii imewezesha wakazi wa Bongi kupata maji safi na salama, hali inayoboresha afya zao, kuongeza muda wa kushiriki katika shughuli za kiuchumi na kijamii, na kupunguza hatari wanazokabiliana nazo wakati wa kutafuta maji.

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

View attachment 3242709
wanashukuru ili iweje wakati ndio kazi ya serikali kuletea wananchi wake maendeleo, nchi hiyi ina viazi wengi sana yaani watu wanashukuru hadi ujinga , kuna limoja nimeona linamshukuru rais kwa kuanguka na pikipiki ila halijaumia SHAME.
 
Wakazi wa Bongi, Handeni walikua wanashida ya maji iliokua ikiwalazima wamama kutembea umbali wa kilomita 3 mpaka 4 ili kufuata maji.

Rais Samia, kama rais wa nchi na kama mama amekua mstari wa mbele kuhakikisha anawashusha wanawake ndoo na kusogeza huduma za maji karibia na maeneo yao.

Rais Samia hafanyi haya Handeni tu, bali amekua kinara wa kuhakikisha maeneo mbalimbali ya ndani ndani ya nchi yanafikiwa na huduma muhimu za kijamii.

Kwa kusogeza huduma ya maji karibu, Rais Samia amehakikisha kwamba wananchi wanapata maji safi na salama, wana muda zaidi wa kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii na hawahitaji kuweka maisha yao hatarini kwa ajili ya kupata huduma za msingi.
 
Back
Top Bottom