KERO Wananchi kata ya Magange wilayani Serengeti kutounganishiwa umeme takriban miaka 6 pamoja na kujaza fomu

KERO Wananchi kata ya Magange wilayani Serengeti kutounganishiwa umeme takriban miaka 6 pamoja na kujaza fomu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ni takriban miaka zaidi ya sita tangu huduma ya umeme ifikishwe katika KATA ya MAGANGE Wilayani Serengeti mkoani Mara lakini tangu wakati huo wananchi mbalimbali walijaza fomu za maombi ya kuunganishiwa lakini mpaka sasa wajapatiwa huduma hiyo.

Baadhi yao walijaribu kwenda mpaka katika ofisi za tanesco mkoa kuulizia hatima ya maombi Yao ya kuunganishiwa huduma hiyo muhimu lakini kero Yao haijatatuliwa Hadi sasa.

Niiombe mamlaka ya usimamizi (TANESCO) Kuwaunganishia umeme waombaji na wahitaji walioko katika Kijiji Cha magange, kata ya Magange, walayani Serengeti mkoani Mara. Maana nani ajuaye gharama za kuunganishiwa umeme wa REA itakuwa kiasi gani mwakani na miaka ijayo?

Huenda wakajikuta (wananchi) wakihitajika kulipia gharama kubwa kuunganishiwa huduma iliyocheleweshwa ilihali kama wangeipata kwa wakati walioiomba wangeipata kwa gharama nafuu na kwa wakati sahihi.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom