DOKEZO Wananchi Kata ya Nyumbigwa – Kasulu tunaishi kwa hofu, kuna raia wa kigeni wanatufanyia ukatili ikiwemo kuhusika na mauaji

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hapa Mkoa wa Kigoma kumeibuka wimbi la mauaji na ukabaji katika Kata ya Nyumbigwa, Wilaya ya Kasulu yanayodaiwa kufanywa na baadhi ya raia wa kigeni wakiwemo kutoka Burundi.

Raia hawa huchukuliwa na baadhi ya wakazi wa hapa Nyambigwa kutoka Makambi ya wakimbizi yaliyopo karibu na eneo letu ili kuwasaidia kazi za shambani.

Hata hivyo, hali imekuwa tishio kubwa kwani baadhi yao wameanza kujihusisha na vitendo vya ukabaji na mauaji ya raia. Hili limekuwa chanzo cha hofu kubwa kwa wakazi wa eneo hili.

Matukio haya yamezidi kuathiri maisha yetu ya kila siku, kwani watu wengi sasa wanaogopa kwenda mashambani kwa kuhofia usalama wao.

Mashamba ambayo ni chanzo chetu kikuu cha chakula na kipato sasa yamekuwa kama maeneo hatari, hali inayozorotesha shughuli za kilimo na maisha kwa ujumla.

Hii imefanya baadhi ya wakazi kuacha kabisa shughuli za shambani na kutafuta njia nyingine za kujikimu, jambo ambalo limeongeza changamoto za kiuchumi.

Tunaomba serikali na vyombo vya usalama kuchukua hatua za haraka kushughulikia suala hili kwani Usalama wetu ni wa msingi, na bila hatua za haraka ili kuhakikisha wakimbizi wanafuatiliwa kwa karibu na wale wanaojihusisha na uhalifu wanachukuliwa hatua stahiki, kwani hili litasaidia kurejesha usalama wa kata yetu na hali ya amani.

Serikali ya Mtaa wanajua kinachoendelea lakini ni kama wanawaogopa Wageni hao, Polisi nao hawajatoa ushirikiano kwetu.
 
Kuna mtu yuko nyuma yao? Maana siku hizi ajira imekuwa ngumu na tamaa ya pesa iko.juu.
 
Back
Top Bottom