Mimi maoni yangu ni kuwa CCM wanajua kuwa bila T-shet, kanga na fedha hakutakuwa na watu. Hivyo wako radhi kuingia gharama kuwabeba kutoka watokako mpaka pale penye kikao ili watakapoiba kura wakashinda waseme "watu walikuwa wengi katika mikutano yetu... oneni". Lakini jana nilikaa kijiweni kwa masaa (kijiwe hicho ni cha washabiki wa CUF) lakini wanamfagilia Dr. Slaa. ila walisema neno moja ambalo linahitaji kufanyiwa Kazi "kama Slaa hashindi mwaka huu, 2015 ni lazima achukue nchi". Maswali yangu yakawa ni .. Kwanini ashindwe mwaka huu? wengine wakasema "Rais ni kila baadsa ya miaka 10! Wengine wizi... Wengine Wapinzani wamegawanyika n.k. Kijana mmoja wa CUF akasema ... CCM hawatujali, badala ya kupunguza kodi kwenye dizeli na mafuta ya taa, wanapunguza kodi kwenye mafuta ya ndege, nani atapanda...? Ni wao wenyewe. Finaly tukakubaliana kuwa Mtanzania yeyote popote alipo, mwenye kadi ya kupiga kura asiangalie chama, angalia mtu mwenye uwezo.
Bado tuna kazi ya kufanya, hata hivyo wananchi wengi wako disatsfied! hiyo ni nguvu kwa Dr. Slaa