[h=2]Wananchi majimbo ya CUF Z'bar waikubali Katiba[/h] Friday, January 23 2015, 0 : 0
[h=1][/h] [h=1]BAADHI ya wananchi waishio katika majimbo yanayoshikiliwa na Chama Cha Wananchi (CUF), wanaiunga mkono Katiba Inayopendekezwa na kusema imetoa jawabu la mambo mengi waliyokuwa wakiyapigia kelele.[/h] [h=1]Wakizungumza na Majira jana kwa nyakati tofauti kwenye Jimbo la Nungwi, Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja, wananchi hao walisema wapo tayari kuipigia kura ya ndiyo.[/h] [h=1]Mkazi wa Shehiya ya Nungwi, Elipokea Mbise alisema Katiba hiyo ni lulu kwa Wazanzibari kwani imebeba mambo mengi ambayo yataifanya Zanzibar ifahamike kimataifa na viongozi wake wa kisiasa kuwa na nguvu Tanzania Bara.[/h] [h=1]"Katiba Inayopendekezwa ni nzuri, imezingatia matakwa ya Wazanzibari katika mambo mengi kama mafuta, kujiunga na mashirika ya kimataifa ili tupate misaada na viongozi wetu kuwa na sauti upande wa Bara, nitaipigia kura," alisema.[/h] [h=1]Mwananchi mwingine, Ali Juma Hamis wa Jimbo la Magomeni, Wilaya ya Mjini, Unguja alisema Katiba Inayopendekezwa ni nzuri na imebeba kilio cha Wazanzibari kwani haikuwa inaliliwa na CUF wala CCM pekee hivyo lazima waiunge mkono.[/h] [h=1]"Katiba hii imepigiwa kelele muda mrefu, tusipoipitisha tutajuta kutokana na uzuri wake...naomba nakala zisambazwe mapema ili wananchi waweze kuipitia kwa kina," alisema.[/h] [h=1]Akizungumza kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, Wilaya ya Kaskazini A, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Bw. Adulrahman Kinana, aliwataka wanachama wa chama hicho kujipanga ili kuipitisha katiba hiyo kwani wingi wao si hoja kama hakuna ushirikiano.[/h] [h=1]"Umoja ni nguvu na wingi si hoja, je, mnataka tuende kwenye wingi si hoja ama kwenye umoja ni nguvu...wingi wetu hautasaidia kama tutashindwa kujipanga, kuhakikisha Katiba inapita," alisema.[/h] [h=1]Aliongeza kuwa, wanaoipinga Katiba Inayopendekezwa ni wale waliotaka Serikali tatu lakini Wazanzibari wengi wanaikubali kwa sababu imezingatia maslahi yao.[/h] [h=1]"Waliokuwa wanataka Serikali tatu walidhamiria kuvunja Muungano," alisema Bw. Kinana.[/h] [h=1]Jimbo la Nungwi linaongozwa na Mbunge wa CUF, Yusuph Haji Hamis, pamoja na mwakilishi wa jimbo hilo Haji Mwadini Makame.[/h]