Wananchi Na Usugu wa Dawa(Drug resistance)

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Siku hizi kila mtu anajua dawa hata kuliko wahudumu wa Afya wenyewe sikatai ni kitu kizuri kuonyesha Sayansi imekua lakini Je kujua kwetu dawa mbalimbali inatusaidia au inazidi kutumaliza zaidi?

Watu wengi sana wametengeneza Usugu wa dawa siku za karibuni kutokana na matumizi yasiokua sahihi ya dawa either mtu anatumia dose chache au anazidisha dawa au anatumia dawa ambayo sio sahihi kwa ugonjwa husika.

Kusikia mtu wa kawaida anakutamkia Powercef inject,Cephalexin Caps,Ciprofloxacine tabs,Ampiclox,Secnidazole...nk ni kitu cha kawaida kabsa wengi wetu tumekuwa tukipenda zile dawa kali kutibu tatizo dogo siku hizi mtu akikohoa kidogo tu keshakimbilia kuchoma powercef/cetriaxone inj tena bila utaratibu maalumu bila kujua kwamba anatengeneza usugu wa dawa mwilini.

Mfano..South Afrika kipindi cha nyuma dawa za Tb zilikua zikiuzwa Kwenye maduka ya dawa na watu kujinunulia wenyewe hizo dawa,asilimia kubwa ya wagonjwa waliishia kupoteza maisha au kutengeneza usugu sugu wa dawa za Tb na kuangukia kwenye group la Chronic cases na Treatment failure ndipo Serikali akachukua jukumu la kugawa dawa za Tb kwenye hospitali.

Tena siku hizi utapata mtu anamuuliza mwenzake wewe ulivyoumwa tumbo ulitumia dawa akijibiwa tu naye anaenda kununua hizo hizo dawa bila hata kipimo chochote bila kutambua tumbo limebeba magonjwa mengi sana anzia Amiba,Uti,typhoid,PUD...nk

Basi ili na Sisi tusifike huko ni vizuri Serikali kupitia Wizara ya Afya kutoa Elimu kwa Wananchi ili kujua hasara za kutumia dawa bila utaratibu mzuri na wananchi wajulishwe ni dawa zipi za kuandikiwa na daktari na zipi za kununua.

Ni hayo tu...Tujenge Tanzania yenye Wananchi wenye Afya Bora kwa Maendeleo yenye Viwango bora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…