Wananchi Nyashimba Waanza Ujenzi wa Shule ya Sekondari Kupunguza Mateso kwa Wanafunzi

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Hatimaye ndoto ya kupata shule ya sekondari ndani ya kijiji cha Nyashimba(M)wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu inaanza kutimia! Baada ya kilio cha muda mrefu kutoka kwa wazazi na walezi, wananchi wa kijiji hicho wameamua kuchukua hatua—kuanza ujenzi wa shule yao ya sekondari kwa kutumia michango ya hiari na nguvu kazi zao.

Kwa muda mrefu, watoto waliomaliza darasa la saba wamekuwa wakilazimika kutembea zaidi ya kilomita 20 kila siku kwenda shule ya sekondari ya Sukuma iliyoko kijiji cha Mwadila. Wengi hushindwa kuhudhuria masomo kwa wakati, na baadhi huacha shule kabisa.


​
 

Attachments

  • IMG_0080.JPG
    1 MB · Views: 35
  • IMG_0065.JPG
    688.5 KB · Views: 25
  • IMG_0006.JPG
    1.1 MB · Views: 32
  • IMG_0012.JPG
    1.2 MB · Views: 30
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…