Pre GE2025 Wananchi takriban 78,000 watarajiwa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura Zanzibar, wanawake wahaswa kujiandikisha kwa wingi

Pre GE2025 Wananchi takriban 78,000 watarajiwa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura Zanzibar, wanawake wahaswa kujiandikisha kwa wingi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wanabodi,

Wanawake visiwani Zanzibar wenye sifa wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura katika zoezi ambalo linatarajiwa kufanyika Febuari Mosi hadi Machi 17, Mwaka huu

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Idara ya Wanawake na Watoto Sitti Abbas Mwinyi katika mkutano maalum ulioandaliwa na Taasisi ya Binti wa Leo ukibeba ajenda mahususi ya kuwahamasisha wanawake kushiriki katika zoezi hilo

Amesema baadhi ya wanawake wengi wanashindwa kujitokeza katika kushiriki kwenye zoezi la uandikishaji hivyo amewataka kuhakikisha wanatekeleza haki yao ya msingi ya Demokrasia

Mwenyekiti wa Taasisi ya Binti wa Leo Nahida Abdalla amesema kujiandikisha kwa wanawake wenye sifa ni takwa la kikatiba ili kutekeleza haki yao ya msingi ya kuchagua na kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba Mwaka huu




Source: Wasafi FM
 
Back
Top Bottom