Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wakuu kuna hii video inako mtandaoni sijajua ni ya lini ila kwa kweli imenihuzunisha sana kwa matendo ya kikatili ambayo wanayapitia hawa Wananchi, na ninadhani huu ni ujumbe mkubwa kwa wenye mamlaka katika nafasi husika.
Soma Pia: Rhoda Kunchela: Askari wa hifadhi wanawafanyia ukatili wa kijinsia wanawake wakati wa oparesheni zinazofanyika hifadhini Katavi
Ndugu na jamaa wa kijiji cha Kisaki mkoani Morogoro wameandamana na kutoa malalamiko mazito dhidi ya askari wa wanyamapori (maliasili) kwa tuhuma za kuwauwa kikatili wananchi wanaoingia msituni kutafuta riziki zao, kama vile kukata mbao.
Mmoja wa wananchi, ameeleza kuwa vitendo hivyo vya ukatili vimekithiri na kuacha majonzi makubwa kwa jamii, huku akiongeza kuwa msituni kuna mafuvu na miili mingi ya binadamu wenzao waliopoteza maisha kwa kupigwa risasi na askari hao
Kulalamikia Watu Kupotea na Kuuawa
Mwananchi huyo anaweka wazi kuwa kuna idadi kubwa ya wenzao wanaopoteza maisha au kutoweka katika mazingira tatanishi.
"Watu wamepotea, watu wanakufa! Acha tuzungumze ukweli... Leo hii wakipotea maana yake kijiji cha Kisaki... sita, nne, kumi, na hao wawili kumi na mbili!. Sijawahi kusikia mwananchi yeyote alienda kwenye mbao akapigwa risasi, sijawahi kusikia"
Kupinga Matumizi ya Risasi Badala ya Kuchukua Faini za Kisheria
Anahoji kwa nini askari wanatumia nguvu ya ziada na silaha za moto kuua watu kwa makosa ya maliasili, wakati kuna taratibu za faini kupitia mifumo ya serikali.
"Faini zipo, wanatakiwa wafanye faini kibao! Mimi mmojawapo nishawahi kukamatwa huku kisa mbao, nikalipia kwenye control number... Anapigwa chuma kwa sababu ya mbao? Anapigwa chuma kwa sababu ya samaki? ... Samaki, mbao, mnauua?!"
Kutishiwa kwa Amani na Kuishi kwa Uoga kama Wanyama
Msemaji huyo anaeleza kuwa ukatili huo unawanyima amani ya kuishi na kujitafutia riziki halali ya kulisha watoto wao, akilinganisha vifo vyao na vya kuku
"Wanakufa kama kuku! Alafu serikali haioni aibu yoyote? ... Hii Tanzania ni nchi ya amani au kisa hiki tunatakiwa tuishi kwa amani au nini hicho kinachoendelea mbele? Kama haitahitajika amani, basi tufahamu! Wa kule wa kule, wa hapa wa hapa!"
Pia soma ~ TANAPA na POLISI wasema wanashirikiana na Wananchi wa Kisaki Morogoro kufuatilia madai ya watu kupotea hifadhini