KERO Wananchi wa maeneo ya Mwakaleli, Halmashauri ya Busokelo tumekuwa tukiahidiwa kujengewa harabara kwa kiwango cha lami lakini haitekelezwi

  • Thread starter Thread starter Anonymous (e941)
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wananchi wa maeneo ya Mwakaleli halmashauri ya Busokelo wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa miaka mingi tumeahidiwa kujengewa barabara kwa kiwango cha lami lakini haitekelezwi.

Ujenzi wa Barabara ya Katumba-Mwakaleli-Lupaso mpaka leo haujaanza licha ya kwamba serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Rungwe mwaka jana April 30, 2024 iliitisha mkutano wa hadhara na kumkabidhi Mkandarasi wa kichina barabara hiyo yenye urefu wa km 35.6

Mpaka leo Mkandarasi haonekani wala hakuna mtambo wowote ulioletwa eneo la mradi.

Ni miezi nane sasa tangu mkataba usainiwe ukimya umetawala licha ya wananchi kubomoa nyumba ili kupisha mradi huo.

Mbunge wa jimbo Atupele Mwakibete Hana akiulizwa anakosa majibu.

Ubovu wa miundombinu ya barabara hii inakwamisha maendeleo ya kiuchumi ya wananchi wa maeneo haya ambao ni wazalishaji wakubwa wa mazao ya kilimo na ufugaji Kama viazi, maziwa, Mahindi, chai na mazao ya misitu.

Tunaomba serikali itusaidie ili Mkandarasi aanze kazi ya ujenzi barabara ikamilike kwa wakati.

 
Ubovu wa miundombinu ya barabara hii inakwamisha maendeleo ya kiuchumi ya wananchi wa maeneo haya ambao ni wazalishaji wakubwa wa mazao ya kilimo na ufugaji Kama viazi, maziwa, Mahindi, chai na mazao ya misitu.๐Ÿ‘Œ๐Ÿฟ
Kaka hivi unalala saa ngapi? Kweli wewe ni mashine sio mtu.
 
Tokeni wote mlale barabarani hadi kieeweke.Wasiwaletee utani.Mbunge wenu ni nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ