Wananchi wa tabaka la chini wazidi kuonewa na umasikini uliokithiri, huku Viongozi wakiendelea kuishi kihafahari kupitia kodi za walala hoi

Wananchi wa tabaka la chini wazidi kuonewa na umasikini uliokithiri, huku Viongozi wakiendelea kuishi kihafahari kupitia kodi za walala hoi

Eric Cartman

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2009
Posts
11,966
Reaction score
11,218
Mazingira ya tulipotokea yanachangia tunapoishia lakini kuna watu wana roho mbaya. Uwezi zuia tamaa za watu wote kwenye nchi ya watu takribani million 50-60 mtu anaekupa hiyo kazi anakuonea.

Lakini wewe kiongozi kwenye nchi ya watu maskini kwa mshahara wako na posho ni zaidi ya millioni kumi kwa mwezi lazima uwe na wasi na watu wako maskini.

Nyumba ghorofa bule

Watoto wako wanasoma private kwa gharama za walipa kodi

Na mambo mengine ya ovyo unayofaidi kwa kodi zao.

Sasa chukulia wewe umetoka familia maskini unaweza vipi kulala kwa amani; wakati umefika hapo kwa madai ya kusaidia watu maskini unasahau vipi ulipotoka.

Unajua uongozi ni dhamana hizi nchi za wenzetu awawezi kukuacha kama ugusi jamii.

Yaani mimi sio kiongozi lakini napata shida nikiona umaskini wa watu wengine mpaka mwili unanisisimuka na siishi kwa kodi zao.

Unakuwaje comfortable na watu maskini bei za bidhaa zikipanda, hao watu wakiwa hawana access na medical care, mazingira ya elimu ovyo.

Seriously mimi naishi kijijini ila siku niliyokuja mjini niliogopa na kuishi kwa kuumia sana mpaka kuna anasa kufanya naona aibu kwa hela niliyoitafuta mwenyewe kutoka kijijini.

Wewe Kiongozi una raha gani unaeishi kwa kodi za hawa watu bila ya mbinu za kuwatoa hao watu walipo.

Aiwezekani sio sawa hawa watu mnaowalelea kuwa viongozi. Aiwezekani mtu raia kama mimi unamuona unajisikia vibaya halafu kiongozi wake aone poa.

The woman has to go; kumvumilia huyu mama ni kiwango chetu cha upuuzi.
 
Watanzania wenzangu nyinyi ni watu wa ajabu sana...hata juzi nilikuwa nawaambia graduate hakuna mwanasiasa yeyote atakaewaonea huruma....mtu kama mwiguru nchemba akuonee huruma wewe!....

Hata mama samia ana watu wake na jamaa zake akina Mohammed chongolo ambao yakiwakuta machozi yanamtoka kwa ajili yao sio mimi na wewe....

Watanzania tuache kulialia ngoma ikiwa ngumu hapa tuhamie sehemu nyingine tukomae mpaka kieleweke.
 
Una elimu duni sana!
Issue sio elimu yangu ata kama ni duni Lakini naona.

Mimi ningekuwa kiongozi nisingeweza kulala kwa amani kwenye geti la askari wakati mitaa michache na nyumba yangu:

Kuna mama anatandikwa na mumewe

Nipite ferry nione mtoto mdogo sijui analala wapi alawatiwe

Nimuone mtu anaangaika kuuza bidhaa nisitafute mbinu za kuakikisha anapata kula ya uhakika

Nione bidhaa zinapanda niache wakati najua wananchi maskini wanaumia.

Na mambo mengine nisikuongopee mimi kama Kilatha nchi kama hiyo ntapigana mpaka naingia kaburini.

Yaani sitoweza kulala kwa amani kama nipo poa. Na nikisema poa yangu ni hela ya kubadili mboga tu.

Especially kwa watoto wadogo yaani nione mtoto wa mchanga mpaka umri wa miaka 16 analala mtaani mjomba huo ugomvi wake auwezi kuwa mdogo kama nina nafasi; yaani mwili unanisisimuka serious nikifikiria how stupid and vulnerable people are at that age.

Labda mi mwenyewe ningekuwa muokota makopo inawezekana ningekuwa na changamoto zingine; lakini kiongozi siwezi vumilia miaka 800.
 
Sawa, hoja yako inasimama. Je tatizo ni huyu woman au hata waliopita?. NB ID YAKO NI YA MUDA HAPA JUKWAANI.
Hiyo sio kwa mtu mmoja ni wote kwa umoja wao ukiwasikiliza they don’t care.

Yaani mtu aumii na vulnerability za mwenzake. Unapo elimika kwa nchi zetu unaona mapungufu ya wasio na bahati kwa angle nyingi;

Unaona mwenzio hajui rights zake kisheria so liwe jukumu lako kumsaidia wewe mwenye elimu.

Mwengine aoni fursa zake za kujiendeleza serikali ilizomuwekea;
Mwelezee fursa zilipo.

Ni jukumu la msomi kuinua jamii iliyomzunguka.

Sasa imagine aina ya viongozi wanaojijali wao awafikirii maamuzi yao yanawaumiza vipi hawa watu.

Nashukuru mungu naweza kimbia kijijini nisione hizi shida za watu; lakini truth be said siwezi kaa kimya ningekuwa mjini penye shida za watu kiongozi awe nani; I just can’t.!
 
Walikuwa wanasema watu wa magufuli wanamhujumu mama

sasa wamechaguana wote wa makunduchi,pwani na tanga line hatusikii kelele ila changamoto zimeongezeka zaidi
 
Brother uongozi ni kitu kigumu sana na pia ni kitu kirahisi sana inategemea na vitu vingi ili kuwa rahisi au kuwa vigumu..

Africa na Tanzania, tunajikita sana kuwalaumu viongozi wetu lakini pia tunasahau maendeleo sio jambo la mchezo mchezo na linahitaji nguvu na akili za watu wooote. JE WATU WOTE WAKO TAYARI KUWEKEZA NGUVU NA AKILI ZAO KWA MUDA MREFU ILI MAENDELEO YAJE KWA MANUFAA YA VIZAZI VIJAVYO?..

Ulaya na America hasa USA hazikuendelea kwa sababu ya akili na nguvu ya mtu mmoja na bado ziaendelea pia sio kwa sababu na akili ya mtu mmoja bali ni KUJITOA (sucrifice ) ya watu wengi wenye lengo moja...

Historia ya Ulaya na USA kufikia maendeleo inapaswa kutupa somo kubwa sana WaAfrica kabla ya kuanza kulaumia wakati hata sisi tunaolaumu hatutimiza wajibu wetu..

JPM akiwa Rais alijaribu kuleta utawala wa kinyapara aka man to man (japo alikuwa na mapungufu yake) ili kila mtu sasa ashiliki kufanya kazi na kuwa na lengo moja kama Taifa, maendeleo maendeleo, kwa wakati huu WaAfrica wanahitaji ukatili ili wajenge nchi zao na then huko mbele woote watajifunza na kukaa kwenye mstari lakini ZILISIKIKA KELELE KILA KONA ZA NCHI NA DUNIA..

Samahani kama niko nje ya maada.
 
Haki ya mungu sisi ni nchi maskini ata waliobahatika wanawajua watu maskini.

Unakuwaje comfortable kama kiongozi wakati umezungukwa na watu maskini.
Honestly kama una ubinadamu na utu, huwezi ku relax ukiwa umezungukwa na watu masikini.

Imagine wewe ni mwalimu wa secondary wa St. Kayumba, maumivu ya kuwaona kila siku watoto wa walala hoi ni makubwa sana, inauma mno. Wakati mwingine hata kuchapa unaona huruma.
 
Back
Top Bottom