Wananchi Wa Venezuela, walaani Bunge lao kutoisimamia serikali na kuitetea, kama chanzo cha uchumi kudorora

Wananchi Wa Venezuela, walaani Bunge lao kutoisimamia serikali na kuitetea, kama chanzo cha uchumi kudorora

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,843
Reaction score
35,442
Wakihojiwa juu ya hali ngumu ya maisha wananchi hao wametupia lawama serikali lakini zaidi wabunge wao kua tatizo.

Wananchi hao Kwa nyakati tofauti wameonesha kukerwa na kuzorota Kwa maisha huku biashara nyingi zikifa kibudu.

Mwanamama mmoja katika mahojiano hayo akiongea Kwa uchungu amesema:

"Tazama waliondoa kipengele cha ukomo wa kukaa bungeni miaka kumi na sasa watagombea milele na kukaa bungeni hadi wafe. Bunge hilo wanachaguana wao na wako wengi wa chama tawala hivo inakua ngumu kututetea wananchi zaidi wanatetea chama chao na familia zao "

Vijana kadhaa wamelaani pia ufisadi kwenye mafuta ambayo makampuni ya viongozi huyauza kimagendo kwenye mataifa mengine, vijana hao pia wamelalamikia ukosefu wa ajira na kulaani zaidi mipango mibovu inayopitishwa na bunge na sera zisizo eleweka dhidi ya taifa lao, Venezuela kumekucha.

Kwa sasa hawamtaki maduro na Spika wa Bunge lao kwa kuunda genge la mafisadi huku wakiteteana.
 
Back
Top Bottom