Wananchi Waaswa Kulitunza Daraja la Berega - Dumbalume

Wananchi Waaswa Kulitunza Daraja la Berega - Dumbalume

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
WANANCHI WAASWA KULITUNZA DARAJA LA BEREGA-DUMBALUME

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Denis Londo ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Kilosa Kijiji cha Berega Kata ya Berege kulitunza na kulilinda daraja la Berega- Dumbalume linalojengwa chini ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(TARURA) amesema kukamilika kwa daraja hilo kutaondoa adha na changamoto iliyokuwepo kwa muda mrefu katika eneo hilo.

Mhe. Londo amesema hayo Juni 23, 2023 akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi unaoendelea katika daraja hilo lilipo Halmshauri ya Wilaya ya Movomero Mkoani Morogoro.

Amesema fedha zilizotumika kujenga daraja hilo ni dhahiri kuwa, Serikali imejipanga kuendelea kuwandoa wananchi wake katika umasikini kwani uwepo kwa miundombinu bora ya barabara inasaidia kurahisisha huduma za kijamii kama hospitali, kuwapunguzia gharama wananchi hasa wanaojishughulisha na biashara za uzalishaji wa mazao kwa kutumia usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine lakini pia kuwapunguzia gharama za kununua hasa zana za kilimo kama pembejeo, mbegu na mbolea.

“Miundombinu ya baraabara ikiwa si mizuri mfanyabiashara yoyote yule lazima apandishe bei kutokana na changamoto ya barabara lakini barabara na madaraja zikiwa nzuri gharama za bidhaa zitapungua wananchi wetu watapata nafuu ya gharama ya maisha sababu wengi wanajishughulisha na kilimo na gharama kubwa ni pembejeo sasa kukamilika kwa daraja hili kwakweli litasaidia kutupunguzia gharama ya vitu sababu ya usafirishaji”

Mhe. Londo ametoa wito kwa viongozi wa eneo hilo kuhakikisha wanalisimamia na kulilinda daraja hilo kwa kutoa elimu kwa wananchi kuepuka kulima na kufanya shughuli zozote hasa zinazoweza kusababisha uharibifu wa mmomonyoko wa udongo ambao unaweza kuharibu kingo na miundombinu ya daraja hilo.

Amesema daraja hilo likikamilika litasaidia usafiri wa wananchi na usafirishaji wa bidhaa kutoka Wilaya za Handeni na Kilindi kwani itakua ni rahisi kwa wananchi kuweza kusafirisha bidhaa na biashara zao kutoka sehemu moja na nyingine.

Awali akisoma taarifa ya mradi Mhandisi Mkazi Bw. David Mwakalalile amesema daraja hilo lina urefu wa mita 140 na upana mita 11 linalojengwa chini ya Mkandarasi Nyanza Road Works Limited Mwanza litaharimu Shilingi Bilioni 7.9 na amesema atasimamia Mradi huo kwa ubora na kukamilika kwa wakati.

Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Kilosa Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa kwa wananchi sio tu kwa usafirishaji wa biashara zao lakini pia kutatua changamoto zilizokuwa zinatokea kwani wapo watu waliopoteza maisha kabla ya kuwepo kwa daraja hilo.
 

Attachments

  • IMG-20230624-WA0017wa.jpg
    IMG-20230624-WA0017wa.jpg
    58.4 KB · Views: 7
  • IMG-20230624-WA0011qawe.jpg
    IMG-20230624-WA0011qawe.jpg
    84.4 KB · Views: 5
  • IMG-20230624-WA0014wqasdrt.jpg
    IMG-20230624-WA0014wqasdrt.jpg
    94.4 KB · Views: 5
Ni kauli za kipuuzi hizi, japo wanasiasa wanazipenda. Hao wananchi wataenda kulitunzia wapi daraja? Majumbani mwao au benki?
 
Back
Top Bottom