Wananchi wa Kijiji cha Ushetu wamemkabidhi zawadi mbalimbali Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani, kama ishara ya shukrani kwa kufanikisha upatikanaji wa huduma ya maji kijijini humo, kilio ambacho wamekuwa nacho kwa muda mrefu.
Katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji uliojengwa kwa gharama ya TZS 192,895,815, wananchi walieleza furaha yao kwa juhudi za Mbunge Cherehani, wakisema amekuwa bega kwa bega na jamii yao kutatua changamoto mbalimbali. Walisema wanamuunga mkono yeye na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zao za kuwaletea maendeleo.
Mradi huo unahudumia vitongoji vinne vya llyamchele, Mwadui A, Igalula, na Sinwankele, ambavyo vina jumla ya wakazi 2,745. Uzinduzi wa mradi huo umeleta matumaini mapya kwa wananchi ambao walikuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji kwa muda mrefu.
Ujinga ujinga tu wananchi umewajaa.mambo ya maji yalitakiwa yawe yameisha kuanzia miaka ya 1970 na ni wajibu wa serikali kufanya Hivyo.Siyo hisani na upuuzi wa kumshukuru mtu.Ni jukumu la lazima ka serikali