mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,126
- 5,068
Dar es Salaam.
Wakati wananchi wakiendelea na kilio cha tozo ya miamala ya simu ambayo ina takribani mwezi mmoja sasa, Serikali imesema bado inalifanyia kazi suala hilo na likikamilika majibu yatatolewa kwa umma.
Tozo hiyo ilipitishwa na Bunge katika bajeti mpya ya Serikali ya 2021/2022, lakini kutokana na kelele nyingi Rais Samia Suluhu Hassan aliahidi Serikali itaifanyia mapitio na kuiweka katika namna nzuri.
Julai 27, Rais Samia akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kuanishwa kwa tozo hizo alisema Serikali inakwenda kuangalia suala hilo njia ya kulitekeleza.
Takribani wiki mbili zilizopita, Waziri wa Fedha Mipango, Dk Mwigulu Nchemba na mwenzake wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile waliwasilisha taarifa ya timu ya mapendekezo ya tozo za miamala ya simu kwa Waziri Mkuu, lakini mpaka sasa inasubiriwa kutolewa taarifa.
Jana, Mwananchi lilimtafuta Dk Mwigulu kujua kinachoendelea, naye alijibu kwa ujumbe wa WhatAspp akisema:
“Jambo hilo bado linafanyiwa kazi, kwenye ngazi ya wataalamu, liliwasilishwa kwenye Baraza dogo la kazi linaloongozwa na Waziri Mkuu Julai 30, kuna maelekezo yalitolewa lifanyiwe kazi zaidi, hivyo lilirudishwa kwa wataalamu.
“Litapelekwa tena kwenye kikao cha kazi baada ya kukamilishwa mtataarifiwa likiwa tayari,” alisema Dk Mwigulu.
Source: Mwananchi