RWANDES
JF-Expert Member
- Jun 12, 2019
- 1,788
- 4,401
Nimetembelea sehemu nyingi za starehe na maeneo mengi ya biashara watu wamejazana na wengine kutovaa barakoa mbaya zaidi wengine walikuwa wakibishana Yanga na Simba jinsi Manara alivyotoka Simba na kuongea na media walikuwa wakitemeana mate hata hawana habari na ugonjwa huo, nilijaribu kuingilia mjadala wao nikagusia kuhusu ugonjwa wa Corona nilichojibiwa nilishangaa sana
Waliniambia Corona haiwezi walipia kodi za majengo wala haiwezi kulipa ada za watoto.
Mbaya zaidi wamesema ni ugonjwa kama magonjwa mengine ukikupata ukifariki ni wewe na maisha yanaendelea!
Nimegusia kuhusu chanjo ya Corona wameniambia hiyo anaijua mkuu wa nchi mbaya zaidi wanasema huwezi kuchanja uendelee kuvaa barakoa kwa hiyo wanasema Mungu ndiye atakayeamua hatima ya gonjwa hili kuondoka nchini
Ndugu zangu katika hali hii Wizara ya Afya bado ina kazi kubwa kuwaelimisha watu ugonjwa huu umekuwa ugonjwa wa HIV maana watu wanashauri kama hujapima na mwenza wako vaa suti lakini waliowengi hawafanyi hivo.
Wananchi wamesema watavaa Barakoa wakienda ofisi za umma maana huko ndio kuna maelekezo lukuki kumbi za starehe hakuna maelekezo hayo