Wananchi wanahitaji kuelimishwa kuhusu Katiba Mpya na sio Maandamano

Maandamano ni haki ya msingi ya kila mmoja wetu,sio kosa kuandamana as far huzuii haki ya asiyetaka kuandamana,KATIBA ni mali ya nchi sio ya chama dola ambacho kimetamka katiba isubiri kwanza!au wewe mtoa hoja hukusikia hili?muda mwingine mtoke huko kwenye comfort zone na mnuse kahawa!
 
Mimi mtu akianza kwa kusema hana ushabiki wa chama chochote ni ishara tosha kuwa ni mfuasi wa Chama Tawala.

Hiyo elimu unayoizungumzia wataitowaje wakati hawaruhusiwi kuwa na mikutano ya aina yeyote inayozungumzia Katiba mpya?

Itakuwaje unaona mapungufu ya Lissu na Mbowe kwenye kupokea maendeleo lakini unafumbia macho waliowaambia raia ambao kodi zao ndio zinatumika kuleta maendeleo kuwa wasipopigia kura chama chao hawatawaletea maendeleo? Ambayo kiukweli si maendeleo bali ni huduma za msingi.

Amandla...
 
Umeelewa mada.?
 
Sasa mbona chadema ndio wanaoonekana wana uhitaji mkubwa wa hiyo katiba kuliko vyama vyote au kuliko wananchi wote.?
 
Mtu kusema hana chama sio dhambi, mimi cjawah kupiga kura wala kujihusisha na mambo ya kisiasa na haitoweza kutokea mimi kuwa na mambo hayo, ila ukweli ni kwamba wananchi wengi hawana elimu kuhusu hiyo katiba mpya na ndio maana muitikio wa katiba mpya inafanywa na Chadema tuu, kama hawaruhusiwi kufanya mkutano bc watafute njia nyingine ila sio maandamano
 
Kudai katiba mpya inatakiwa ubebe bendera ya nchi na sio bendera ya chama cha siasa.
 
Kwani toka lini maana ya sentesi "Kongamano la Katiba Mpya" imekuwa "Maandamano ya Katiba Mpya"?

Hebu tuanzie hapo, tufafanulie hilo kabla hatujakuambia wewe ni nani; tupe tofauti ya Kongamano na Maandamano

Inawezekana ukawa mtani wangu Msukuma wewe kwako kongamano na maandamano ni baba mmoja, vinaingiliana moja kwa moja!
 
Maandamano ni baada ya kuzuiwa kufanya mikutano kwa ajili ya kuelimisha wananchi. Mikutano isingezuiwa wasingeitisha maandamano. Sasa badala ya kuwalaumu ambao hawataki wananchi waelimishwe wewe unawalaumu wanaotaka kuwaelimisha! Hiyo ndio definition ya unafik.

Amandla...
 
Ukitaka upewe elimu je serikali ya CCM sio hiyo hiyo inazuia makongamano??

Kwenye makongamano huko ndio elimu ingetolewa kwa uzuri pia ila nayo yamekua banned

Elimu ipo pia mtandaoni kule kwenye space ya twitter ila serikali hiyo hiyo ya CCM iliyofungia twitter miezi zaidi ya 5 bado inaslow internet watu wasipate elimu maana leo hii mitandao ndio imefanya dunia kuwa kijiji..

Mwisho ni kusema Jiwe alishindwa nini kuanzisha ufindishaji wa katiba shuleni badala yake bila kushauriana na wataalam akajianzishia somo la historia feki inayomsifu kuwa ndio Rais aliyefanya makubwa kuliko wote.

Kwa kifupi CCM hawako tayari kusikia watu wakipewa elimu kuhusu katiba hasa ukizingatia madhaifu lukuki iliyonayo katiba hiyo

Tafakari hayo!
 
Kongamano ni mkutano na maandamano ni katika kuhitaji kitu fulani
 
H
Hueleweki lengo la uzi wako. Ni kumpoda Lisu na Mbowe, au kuzungumzia uhitaji was katiba mpya, au elimu ya uraia. Sio kazi ya Chadema kutoa elimu ya uraia. Vinginevyo kamwamboe m/kiti wako ccm itoe elimu hiyo. Maandamano ni haki kikatiba kwa anaetaka/wanaotaka kuandamana kushinikiza au kuonyesha hisia zake/zao ktk Jambo fulani. Andiko la linakuweka wazi kuwa wewe Ni mwanachama au shabiki waa ccm, usione haya kujibainisha, au acha unafiki.
 
Popo: Ni mnyama au Ni ndege?
 
Kama chadema waliweza kuwashawishi watu wasipokee vitu kutoka serikalini kwann wanashindwa kuwashawishi kukubali katiba mpya.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…