Wananchi wanategemea Demokrasia iwapatie maisha bora

Wananchi wanategemea Demokrasia iwapatie maisha bora

Maingu Ernest

New Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
1
Reaction score
0
Wananchi wanaunga mkono demokrasia si kwa sababu ni kitu muhimu kwa chenyewe, bali pia wanatarajia demokrasia iwapatie maisha bora ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Hili lilionekana wazi sana wakati wa maandamano ya mapinduzi nchi za Uarabuni mwaka 2011, pale watu wengi walipomwagika mitaani na kwenye viwanja mbalimbali ili kushinikiza serikali zao kuwapatia mahitaji
yao muhimu na haki za binadamu (huku wakiimba, kwa mfano, kwa kaulimbiu kama vile “mkate, uhuru na utu”).

Watu wanatarajia serikali zao kutoa huduma za umma kwa ufanisi mkubwa ambao utakidhi mahitaji yao na kutambua haki zao kama binadamu. Watu wanatarajia kuwa na uwezo wa kusema kero zao na kuweza kusikilizwa na mamlaka husika.

Mwongozo huu unajenga hoja katika wazo la uwajibikaji wa kidemokrasia kwa kuingiza mawanda ya kisiasa ya utoaji wa huduma kwenye mjadala ambao kimsingi ulilenga kuchocheo mabadiliko ya kijamii. Serikali zinazowajibika kwa wapiga kura, au wawakilishi na vyombo vya usimamizi, kama vile bunge, vyama vya kisiasa au taasisi kuu za ukaguzi wa hesabu—zenye uwezo wa kuzishawishi taasisi hizo, ina uwezo wa kutimiza matakwa ya wananchi kuliko serikali ambazo haziwajibiki. Ni katika mfumo wa kuchunguzana na kukaguana kidemokrasia ndipo uwajibikaji unaweza kuwa chombo cha mabadiliko katika utoaji wa huduma.

Utafiti unaonesha kuwa nchi zenye viwango vya chini vya utoaji wa huduma zinafanana katika jambo moja: hazina sheria au zina sheria dhaifu katika kuwapa adhabu au kuwapa tuzo wale wanaofanya vizuri (International IDEA 2013a).

Mwongozo wa tathmini umelenga kujenga mahusiano kwa kuwaunganisha mtu mmoja mmoja, wawakilishi wao wa kuchaguliwa na dola, ikiwa ni pamoja na kwenye ngazi ya kitongoji, ambako huduma za umma zinatolewa, kwa njia zinazotimiza haki za binadamu za wanaume, wanawake, wavulana na wasichana. Kwa maana hiyo mfumo wa tathmini umelenga zaidi kuongoza zoezi la
tathmini, maana ni njia ya kushauriana na kubuni hatua halisi za kuimarisha uwajibikaji wa kidemokrasia katika utoaji wa huduma.

Mfumo wa tathmini unalenga kuimarisha uwajibikaji wa kidemokrasia (yaani; uwajibikaji wa kijamii na wa kisiasa) katika utoaji wa huduma katika nchi zenye demokrasia iliyokomaa au demokrasia inayoibukia.

Kwa kuwa lengo kuu la demokrasia ni mchakato wa kufanya maamuzi kuwa katika udhibiti wa wengi na kuleta usawa wa kisiasa, Taasisi ya Kimataifa ya Demokrasia na Msaada katika Uchaguzi (International DEA) imeandaa mbinu inayoruhusu ushiriki mpana wa watu na mchakato shirikishi wa tathmini unaofanywa na kumilikiwa na wananchi wa maeneo husika. Mbinu shirikishi kimsingi ni muhimu sana kama matokeo ya tathmini yalivyo muhimu.
 
Back
Top Bottom