Wananchi waukataa Muungano wa Serikali mbili

Wananchi waukataa Muungano wa Serikali mbili

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Huu ni utafiti usio rasmi! Yeyote mwenye mashaka aingie "field" kujiridhisha.

Watanganyika hawautaki kwa sababu hawakushirikishwa. Rais wao wa wakati huo alijiamulia mwenyewe bila kujali matakwa ya wananchi wengi.

Wazanzibar ndiyo kabisa, hawataki hata kuusikia. Nao kama wangeshirikishwa inawezekana wasingeukubali.

Kwa ufupi, ni viongozi wa Tanganyika na Zanzibar ndiyo walioungana na si nchi zao wala watu wao! Ndiyo maana imeshindikana kuuzika Uzanzibar na Utanganyika.

Mitazamo ya sasa kwa kada tofauti kuhusiana na Muungano:

1. Watanganyika: Serikali moja, au Serikali tatu, au kila mmoja abaki na nchi yake

2. Wazanzibar: Serikali tatu au Muungano uvunjwe

3. Watawala Watanganyika: Serikali mbili, ikishindikana, basi Serikali moja.

4. Watawala wa Zanzibar: Serikali tatu au Muungano uvunjwe.

5. Wasomi: Serikali tatu.

6. CHADEMA, ACT WAZALENDO, CUF, NCCR MAGEUZI na vyama vingine vya upinzani: Serikali tatu

7. CCM: Serikali mbili au moja na si vinginevyo

Kwa sura hiyo, ni wazi kuwa Watanganyika na Wazanzibar hawautaki muundo wa Muungano wa sasa wa Serikali mbili. Ili Muungano uendelee kudumu, sharti hitaji la wengi lizingatiwe: Serikali tatu.

PIA SOMA
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?
 
Mimi nashauri uvunjwe tu
Ukivunjwa Muungano Leo Rais Samia Atakuwa rais wa nchi Gani?? Alichaguliwa na Wtz NayoTz haipo tena Imekufa!;
Rais Mwinyi Ataendelea Kuwa Rais wa Zenj sababu Alichaguliwa na waZenj
 
Muungano wa Shirikisho

Kimsingi huu ni muungano wa Serikali 1 kwa sababu SMZ haitambuliwi popote duniani 🐼
Inatambulika Tanganyika. Hayo mengine ni mambo ya kisiasa tu, hayana manufaa kwa wananchi wa Taifa la Zanzibar.
 
Sahihi

Na watanganyika walishirikishwa kupitia wabunge wao kupitisha mambo ya muungano

Sababu uliridhiwa na bunge
Muungano wa nchi 2duniani kote huridhiwa na wananchi kupitia kura ya maoni sio wabunge km ilivyofanyika ,wananchi ndo wenye nchi sio Nyerere wala wabunge wa ccm wa wakati ule
 
Back
Top Bottom