SoC02 Wanandoa kuanza kulipwa pesa ya kujikimu ili kuokoa single mama na taasisi ya ndoa Tanzania

SoC02 Wanandoa kuanza kulipwa pesa ya kujikimu ili kuokoa single mama na taasisi ya ndoa Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Thailand

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2019
Posts
275
Reaction score
795
salama!
Niende kwenye mada kwa kuanza na maswali ya utangulizi.
  1. Ni kwa namna gani unavyoshuudia idadi ya watoto wa kike wakipewa mimba na kutelekezewa watoto na waume zao?
  2. Ni kwa namna gani vijana wa kiume wanakimbia suala la kuoa ( kuweka wake ndani) kwa kisingizio cha ugumu wa maisha?
  3. Ni kwa namna gani vijana hao hao wa kiume wanaongoza kupiga miti watoto wa kike (ngono zembe) lakini likija suala la mimba wanatoka nduki?
Kujibu hayo maswali inaonesha namna kabisa taasisi ya ndoa na malezi ya watoto itakavyo pata mushikeri huko siku za mbeleni kama hakutakuwa na njia yoyote ya mapema kuokoa taasisi hii.

Hivi fikiria mzazi umejipinda kusomesha mtoto wako wa kike kwa tabu mpaka anamaliza chuo, then anapigwa mimba akiwa kwako nyumbani then bwana wake anashindwa kumchukua kisa ugumu wa maisha kijana wa kiume, bado alikuwa ajajipanga.
Sasa ili kuokoa taasisi ya ndoa jamii tuungane kusaidia vijana walio kwenye ndoa Pesa ya kumudu maitaji yao.
Kwa sababu hata pasipo kuwasaidia vijana wataendelea kuzalisha watoto wa kike na watakao baki na msalaba huo ni wazazi wa binti huyo na huyo mtoto atakae zaliwa hapo.
Sasa nini cha kufanya;
  1. Serikali kupitia pesa za tozo inazokusanya iweke angalau 2% tu kwenda kwenye mfuko wa familia hasa ndoa changa ili zijikimu juu ya ugumu wa maisha ambao kwa kiasi kikubwa ndo unapelekea kuachana kwa ndoa nyingi,
  2. Lakini serikali bado ina rasilimali nyingi hapa nchi Tanzania kama migodi, hifadhi ya misitu, maji au wanyamapoli serikali inaweza tenga hifadhi moja kwa ajili ya kuratibu (finance) jambo hili
  3. Familia zitapewa kama shs 500,000 kila baada ya miezi mitatu au miwili ili kuwajengea sense ya kujitafutia pesa zao wenyewe
  4. Familia itapokea pesa hii ni mke na mme kwa pamoja wenye nyeti cha ndoa na uthibitisho kwamba wapo pamoja kwenye nyumba moja
  5. Malipo haya yatafanyika kwa kipindi cha miaka 10 au 20 tangu ndoa kufungwa
Faida ya mpango huu:
  1. Taasisi ya ndoa hasa ya vijana wetu hawa wadogo itadumu sana kwenye mahusiano
  2. Single mama watapungua kwa sababu vijana wengi hawatawanya wake zao kirahisi kisa ugumu wa maisha.
  3. Watoto wanaotelekezwa na wazazi wao kwenye vituo vya kulea watoto na kwa bibi zao itapungua sana na hivyo watoto watakuwa na uhakika wa malezi bora kutoka kwa wazazi wao wote wawili (baba na mama)
  4. Ustawi wa taifa letu utaendelea sana kwa sababu tutakuwa na jamii inayooungana kwenye malezi ya watoto wao.
  5. Uchimi wa taifa utakuwa kwa sababu wawili hawa watatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuendeleza familiao yao kwa sababu pesa hii ya kujikimu haitolewi kila mwezi hivyo kwa vipindi ambavyo hawapokei pesa hiyo watabidi kufanya kazi ya uzslishaji ili kupata pesa ya kuhudumia familia yao.
Muamal Gadaffi aliweza kufinance vijana wa Libya walipokuwa wakiingia kwenye taasisi ya ndoa, sisi watanzania tunaweza kufanya jambo hilo kwa uzuri kabisa kama kwa pamoja tutaitaji kuinua na kuboresha taasisi ya ndoa kwa vijana wetu wanaoitaji pesa na elimu zaidi juu ya mahusiano na mstakabali wa ndoa zao
 
Upvote 0
Pia usisite Kutoa maoni juu ya andiko hili.
Kulipigia kura kwa kugusa kialama ^ pembeni ya tarakimu na neno votes.
Pia, usisahau kulike andiko hili
 
Back
Top Bottom