Wanandoa kuweni makini.

Vituka

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2011
Posts
2,266
Reaction score
1,264
Kwa wale Wakristu nadhani mnafahamu kuwa Ndoa (iundayo familia) ni taasisi muhimu sana katika Kanisa na ni nguzo kuu ya Kanisa. Kwa nini? Katika ndoa ambayo huunda familia ndiko Kanisa linakoanzia, hapo tunapata Mapari, masista, wachungaji, e.tc. Pia katika ndoa tunapata wataalamu mbalimbali kama walimu, doctors, engineers e.t.c. Hao wote kwa pamoja ni watu muhimu sana katika Kanisa na jamii kwa ujumla wake.

Sasa basi, the DEVIL wants to destroy everything planned by God, so has started at the grass roots, na hii ni NDOA. Ndiyo maana humu JF kila kukicha wanandoa wanalia na kulalamika. Ndoa hazina amani wala upendo, zimekosa uaminifu, makahaba na mashoga wameziingilia ndoa hizi!Yani mashambulizi ya shetani yamehamia zaidi katika taasisi hii nyeti iliyoundwa na Mungu kwa makusudi mazima ya kuliendeleza Kanisa na kujenga jamii imara.

Wapendwa, mlio katika ndoa na mnaojiandaa kuingia katika ndoa, mjue kuwa shetani anawatamani sana, na anataka aharibu kile Mungu alichokipanga kupitia kwenu ili kulijenga kanisa na jamii nzima. Kila jaribu au kikwazo kitakachowapata, fahamuni kuwa mnarushiwa shambulizi na shetani kusudi msiwe na amani, mfarakane na hata muachane ili yeye atimize lengo lake kuu ambalo ni kuliharibu Kanisa la Mungu na yeye atawale Dunia.

Kuweni makini sana wanandoa, na mnaojiandaa kuingia katika ndoa, mshikeni sana Mungu ili awaepushe na huyu mwovu na mwisho mlijenge Kanisa la Mungu.

TAKE CARE!
 
Hili ni suala nyeti sana lakini watu wanalichukulia poa sana!
 
By Eiyer
Hili ni suala nyeti sana lakini watu wanalichukulia poa sana!

Mkuu kweli umenena, people kuweni mkini!Kila siku takuwa mnagombana hadi mnakosa muda wa kutafuta watoto, ohoo!shauri yenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…