Wanaoamini hakuna Mungu wana hoja, wasikilizwe

Wanaoamini hakuna Mungu wana hoja, wasikilizwe

comrade_kipepe

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2019
Posts
3,411
Reaction score
4,435
Hawa watu msiwatukane, wasikilizeni maana Wana maana Yao kusema hivyo, wengi wao wanaoamini hivyo wameamua kua hivyo kutokana na magumu na machungu waliyokutana nayo kwenye maisha na walipomuhitaji Mungu hakuwasaidia.

Unakuta mtu ana jambo linalomnyima furaha kwenye maisha, ametafuta msaada kwa MUNGU nae hajamsaidia, sasa mtu anashikwa na gadhabu " Kweli huyu Mungu kama yupo kwanini hanisaidii kwenye hili? Na tunaambiwa NI Mungu muweza wa yote"

Unajua kuna mengi Sana yanaendelea kwenye hii Dunia unajiuliza Mungu anaona kweli? Na kama anaona mbona hazuii haya?

Kwa mimi naona hawa Atheist ⚛️ Wana hoja wasikilizwe, Mimi binafsi sio Atheist lakini kuna mambo yanatokea kila kukicha naona kama mbona kama hawa jamaa Wana hoja? Yani kila siku zinavyoenda naona kama hawa jamaa wana point.

Binafsi napata utata, siamini kama Dunia ilitokea tuu from no where, naamini lazima alikuwepo muumbaji lakini wasiwasi wangu NI KWELI HIZI SIFA ZA HUYU MUUMBAJI "Mungu" tunazozisikia na kuzisoma zina ukweli?

Je, Mungu ana huruma kweli? Mbona yanayoyokea sioni kama kweli ana huruma na watu wake?

Mimi naona Ni

*Mbinafsi
*Hana huruma
*Kiburi
*Kuna mambo yako nnje ya uwezo wake
* Ana upendeleo

Au nawaza baada ya kuumba ulimwengu na vilivyomo, yeye akamtupa shetani na majini duniani Sisi binadamu wake anaotupenda tupambane, halafu yeye akakaa pembeni!?

Nataman sana niabudu DINI za asili ambazo zilikuepo kabla ya ujio wa waarabu na wazungu, lakini nashindwa nianzie wapi Mimi Nina asili ya Kagera japo sipajui.

Kwa sasa nikiona mtu anaenda kanisani Yani naona kama ametoka kudanganywa 😀 sijui nimeshaathirika kisaikolojia, kanisani sijawah kukanyaga mwaka wa 15 huu (lakini cha kushangaza Mimi ni mtu mwema kuliko hata hao wanaojazana kanisani maana wengi nakaa nao huku mtaani, wengi walevi tuu na wanapenda sana ch*pi!

Nipe muongozo wakuu kua muumini wa DINI za asili kabla ya ujio wa waarabu na wazungu naanzia wapi?
 
Hio system IPO tuma advansi
FB_IMG_1725728286396.jpg
 
jina lako limetosha kujibu ulichoandika! unahitaji fikra kidogo tu kujua upuuzi ulioandika!.
😂😂.kwa akili zako unadhani Mungu anataka nini kwako?au anakutegemea kwa lipi?.wala hana haja na wewe
 
Suala sio kuamini Mungu yupo au hayupo issue wathibitishe huyo mungu anafanyaje kazi zake vipi, na walimuona wapi? Kunieleza uamini kitu haukuoni napo ni kukosa akili
 
Zile amri kumi wanazoita za mungu ni natural community rules zilizotumiwa na jamii mbalimbali kuongoza jamii zao
 
Suala sio kuamini Mungu yupo au hayupo issue wathibitishe huyo mungu anafanyaje kazi zake vipi, na walimuona wapi? Kunieleza uamini kitu haukuoni napo ni kukosa akili
Anapohitajika atende hatokei, hatendi, kazi kazi zake anafanyaje
 
Mungu yupo makaburini?
Yupo kila sehemu. Ila utaanza kuona uwepo wake siku unapoanza kukata mawasiliano ya dunia.na kuanza kwenda ulimwengu mwingine. Na kuona viumbe tofauti na uliowazoea.ndo utajua ehee kumbe kweli.sasa kurudi duniani unashindwa unabaki NA LAITI NINGEJUA.ila unakuwa umeshachelewa
 
Hakuna kitabu au vitabu vilivyoshushwa kutoka mbinguni hapo pia mlipigwa, zile ni story na hadithi za watu wa jamii mbalimbali zenye masimulizi tofauti kulingana na nyakati zao katika maisha
 
Namimi hapo nilishaandika juu kua ana Sifa ya "kiburi"
Hapana NI MPOLE ndo maana anakuacha ufanye unavyotaka.anakupa pumzi,anakupa riziki amekuweka ndani ya tumbo la mama yako miezi 9.ukiwa shahawa za baba yako ukabadilika ukawa mtu.angekuwa na kiburi angekupoteza huko huko.ulipo kuwa zamani.dingi yako angekula nyeto ukapotea
 
Hawa watu msiwatukane, wasikilizeni maana Wana maana Yao kusema hivyo, wengi wao wanaoamini hivyo wameamua kua hivyo kutokana na magumu na machungu waliyokutana nayo kwenye maisha na walipomujitani Mungu hakuwasaidia.

Unakuta mtu ana jambo linalomnyima furaha kwenye maisha, ametafuta msaada kwa MUNGU nae hajamsaidia, sasa mtu anashikwa na gadhabu " Kweli huyu Mungu kama yupo kwanini hanisaidii kwenye hili? Na tunaambiwa NI Mungu muweza wa yote"

Unajua kuna mengi Sana yanaendelea kwenye hii Dunia unajiuliza Mungu anaona kweli? Na kama anaona mbona hazuii haya??

Kwamimi naona hawa Atheist ⚛️ Wana hoja wasikilizwe, Mimi binafsi sio Atheist lakini kuna mambo yanatokea kila kukicha naona kama mbona kama hawa jamaa Wana hoja? Yani kila siku zinavyoenda naona kama hawa jamaa wana point.

Binafsi napata utata, siamini kama Dunia ilitokea tuu from no where, naamini lazima alikuwepo muumbaji lakini wasiwasi wangu NI KWELI HIZI SIFA ZA HUYU MUUMBAJI "Mungu" tunazozisikia na kuzisoma zina ukweli?

Je Mungu ana huruma kweli? Mbona yanayoyokea sioni kama kweli ana huruma na watu wake?

Mimi naona Ni
*Mbinafsi
*Hana huruma
*Kiburi
*Kuna mambo yako nnje ya uwezo wake

Au nawaza baada ya kuumba ulimwengu na vilivyomo, yeye akamtupa shetani na majini duniani Sisi binadamu wake anaotupenda tupambane, halafu yeye akakaa pembeni!?

Nataman sana niabudu DINI za asili ambazo zilikuepo kabla ya ujio wa waarabu na wazungu, lakini nashindwa nianzie wapi Mimi Nina asili ya Kagera japo sipajui.

Kwasasa nikiona mtu anaenda kanisani Yani naona kama ametoka kudanganywa 😀 sijui nimeshaathirika kisaikolojia, kanisani sijawah kukanyaga mwaka wa 15 huu ( lakini cha kushangaza Mimi ni mtu mwema kuliko hata hao wanaojazana kanisani maana wengi nakaa nao huku mtaani, wengi walevi tuu na wanapenda sana ch*pi!

Nipe muongozo wakuu kua muumini wa DINI za asili kabla ya ujio wa waarabu na wazungu naanzia wapi??
Na wewe pia una hija usikilizwe.

Ndio maana watu wanatuteka tu na kutuua wanavyotaka walishajua hakuna kitu kinaitwa Moto wa Jehanamu wala Mbingu.
 
Duniani Kwa sasa hakuna nabii, mtume, padre, sheikh, mchungaji wala yeyote ambaye atakuja kua msaada kwako hayupo na hata miujiza unayoona ni mazingaombwe na utapeli wa wazi
Na vipi kuhusu mungu
 
Back
Top Bottom