albuluushiy
JF-Expert Member
- Oct 2, 2013
- 1,404
- 686
"Based on criminal law these individuals are sentenced to the severest punishment which is death sentence" Hivyo ndivyo Jaji Safihullah Mujadidi, alivyotoa hukumu ya kifo kwa wanaume saba. Nao mtandao wa Mail Online kutoka Uingereza ukaandika: Seven Afghan men sentenced to death for gunpoint gang rape of four women – including one who was pregnant. Nayo pia redio Swahili- Tehran ikasema, mahakama moja huko Afghanistan imetoa hukumu ya kifo kwa watu saba baada ya kupatikana na hatia ya kuwabaka kwa pamoja wanawake wanne.
Katika kesi hiyo iliyochukuwa muda wa saa chache tu mahakama ilielezwa kwamba katika tukio lililojiri tarehe 23 ya mwezi uliopita wa Agosti, watu hao, huku wakiwa wamevalia sare za polisi na kubeba bunduki waliusimamisha msafara wa magari yakitoka harusini na kuelekea mji mkuu wa nchi hiyo Kabul. Kisha wakawaburuza wanawake wanne kutoka ndani ya gari hizo, wakawapora vito vya thamani, wakawapiga na kisha wakawabaka.
Imeripotiwa kuwa mmoja wa wanawake hao alikuwa ni mja mzito. Hayo ni ya huko Afghanistan, mijitu mizima inabaka wanawake. Usishangae ukiambiwa kuwa watu hawa na vitendo vyao hivyo viovu lakini wameshaoa na wana watoto. Ukielezwa hilo usishangae, japo sina ushahidi na hilo. Lakini ni dhahiri kuwa baadhi yetu tumekosa utu. Wakati hayo yanatokea, nalo Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limelituhumu jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia kuwabaka wanawake wenye matatizo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wahanga wengi wa ubakaji huo ni wakimbizi waliokimbia maeneo yao ya vijijini wakati wa njaa kubwa mwaka 2011 na kuhamia katika kambi kwenye mji mkuu, Mogadishu. Waandishi wa ripoti hii walitumia ushahidi wa wanawake 21, ambao walisema kuwa wakati mwingine wanajeshi hao wa AMISOM hutumia fadhila kama vile chakula cha msaada kuwalazimisha kufanya nao ngono.
Wasichana hao pia waliiambia Human Rights Watch, kwamba wakati mwingine wanajeshi hao waliwashika kwa nguvu wanawake waliokwenda kwenye kambi zao kutafuta huduma ya maji au huduma za matibabu. Mhanga mwenye umri mdogo zaidi ni mwenye umri wa miaka 12 alisema alibakwa na mwanajeshi kutoka Uganda.
Inasikitisha sana kuona wale waliopelekwa kutuliza hali ya mambo Somalia wanafanya haya. Napata wakati mgumu sana wa kufikiria wanawake wa Kisomali wanaobakwa na wanajeshi wa AMISOM. Hadi watoto wa miaka kumi na mbili nao wako katika dimbwi la unyama wa kubakwa. Sijui tunataka watoto wa Mama hawa wao wafanye nini! Unaweza kumlaumu mtu kuwa anafanya uovu lakini kumbe wewe ndio umeanza uovu, yeye anamalizia tu.
Umemwaga ugali anamwaga mboga. Wametoka katika nchi zao Kenya, Uganda n.k. Lakini mambo wanayoyafanya kule ni ya kusikitisha sana, na wala hii si mara ya kwanza au ya pili. Hata vyombo vya uslama vya Kenya navyo vilituhumiwa kufanya ubakaji na udhalilishaji kwa Mama wa Kisomali wakati wanawahamisha kutoka Kenya kuwarudisha Somalia tena kwa nguvu. Ni nadra habari kama hizi kuzisikia, kwa sababu huwa wanaficha uovu wao. Lakini ukweli utabaki kuwa AMISOM wamekuwa wakifanya vitendo viovu Somalia na hata wakati mwengine wanauwa watu wasiohusika lakini habari kama hiyo hutoisikia ikipeperushwa hewani.Ni adimu sana!
Nimepata nafuu kuwa wale wabakaji wa kule Afghanistan wamehukumiwa kifo na hata Rais wa nchi hiyo Hamid Karzai, amegongomelea msumari na kusema kuwa ni lazima wanyongwe. Lakini napata wasiwasi juu ya hawa AMISOM, kuwa hizi tuhuma huenda zikaishia tu hivi hivi na wala hakutokuwa na uchunguzi. Sijui kubaka ndio sehemu ya majukumu yao katika kazi zao. Sidhani hivyo, lakini ni ushenzi tu walionao baadhi ya binaadamu.
Kwa mujibu wa Reauters, ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imegundua kwamba, kando na kuwepo watoto wa kike takriban milioni 120 ulimwenguni, mmoja kati ya kumi wanabakwa au kudhalilishwa kingono hadi wakati wanapofikia miaka 20. Katika utafiti uliofanywa juu ya unyanyasaji dhidi ya watoto, shirika hilo linaloshughulikia masuala ya watoto UNICEF limesema asilimia 20 ya waathiriwa wa mauaji ni watoto walio chini ya miaka hiyo 20.
Mauaji ni sababu kubwa ya vifo miongoni mwa watoto wa kiume na vijana wa kiume walio na miaka 10 hadi 19 katika mataifa ya Amerika ya Kusini, yakiwemo mataifa kama Venezuela, Colombia, Panama na Brazil. Mkurugenzi wa UNICEF Anthony Lake anasema; "Hizi ni habari za uhakika zinazotia wasiwasi sana, hakuna serikali au mzazi anayetaka kuviona visa hivi" Hakuna serikali au mzazi anayetaka kuviona visa hizi, huu ni ukweli usiopingika lakini cha kusikitisha na kuumiza hao wazazi ambao hawataki vitendo hivi viwepo ndio hao hao baadhi yao wanaovitekeleza. Hutaki mwanao abakwe. lakini kwanini unabaka watoto wa wenzako? Napenda sana kusema kuwa kipimo kizuri cha kutaka kumfanyia mwenzako uovu, kwanza jiulize hili jambo nikifanyiwa mimi nitafurahi? Unataka kubaka Mama wa Kisomali, Mama yule kazaa ana watoto wa kike na kiume kama wewe na pia ana wajukuu.
Sasa jiulize Mama yako mzazi akifanyiwa vile, jee wewe utakuwa radhi! Unataka kubaka mtoto wa mtu, jee kwa mtoto wako itakuwa vizuri kwako? Ukiletewa taarifa kuwa mtoto wako kabakwa na wanaume saba. Utajisikia vizuri? Ikiwa hujisikii vizuri basi usifanye uovu kwa watoto wa watu wengine. Ni jambo la kukaa kitako na kulifikiria, lakini siku zote wapo baadhi ya watu huwa hawasikii wala kuona japo wana macho na masikio. Hata kufikiria hawafikirii japo wana ubongo.
Ukiyafikiria haya naamini huwezi kubaka mtoto wa mtu ama Mama wa mtu, lakini fikra hizi ziko umbali mkubwa na akili za wabakaji. Hii ni sawa na kile kisa cha mtu mmoja aliyekwenda kwa Mtume na kumwambia kuwa naweza kuacha dhambi zote lakini dhambi ya zinaa hawezi kuiwacha na akamtaka Mtume kwa dhambi hiyo amruusu aendelee nayo. Alipokuja ukilizwa juu ya hao anawao-wazini kuwa si dada na Mama za watu! Suali lilipokuja kuwa kama kuna mtu anafanya zinaa na Dada ama Mama yake, yeye atajisikiaje? Baada ya kuyaweka haya kichwani na kufikiria mara mbili aliona kuwa ni kweli, wakwangu mimi wakifanyiwa haya basi roho yangu haitokuwa safi na nitakuwa tayari kwa vita.
Siku zote wenye akili ndio wafikiriao, aliamua kuiwacha dhambi ya zinaa kwa sbabu hataki watu wake yawatokee. Nasi tunatakiwa tuwe hivi, lisilokuridhi kufanyiwa basi usimfayie mtu mwengine. Wema hauozi na mlipaji hafi kama ulivyo fanya ndivyo utakavyo fanyiwa. Ikiwa ulimbaka mtu mukiwa watatu basi huenda wako akabakwa na sita, ikiwa ulimbaka mtoto wa mtu wa miaka 12 hueda wa kwako akabakwa akiwa na miaka 6 tena na watu wawili.