Wanaobeba vifurushi mgongoni huku wakiomba barabarani huwa wanabeba nini?

Wanaobeba vifurushi mgongoni huku wakiomba barabarani huwa wanabeba nini?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Katikati mwa miji nakutana na wabibi wengine wanakuwa ombaomba wamefunga mizigo mgongoni ni kama vipande vya nguo kwenye kanga unakuta anatembea nao huo mzigo mchana kutwa, ile inakuwa ni kitu gani? Mbona kama ni mambo ya kishirikina wanakuwa nayo?

Mimi naogopa sana kumsaidia bibi wa namna hiyo na kuna wale wengine watoto wenye ulemavu wa akili unawakuta stand au sokoni wanaomba mpaka unajiuliza huyu anatumiaje hela, ananunua kitu gani?

Maana kwa hali aliyonayo hata msaada wa chakula atapewa bure na mama ntilie wale itakuwa wanatumwa na watu wakubwa, wamegeuzwa kama misukule.
 
Jana nimeona wawili mmoja kachoka zaidi, mwenye nguvu kias ndo kamshika mkono mwenzio wanaomba omba madukani
Dar wako sana mitaa ya mnazi mmoja maeneo ya kitumbini pale...kwa tafiti tulizofanya wengi wao si kwamba ni ombaomba per se! wengi wao wana miliki nyumba zaidi ya moja maeneo tofauti ya mji! Wengi wanadai kuomba ni mazoea yao!..
 
Kuna mbibi alivaa ushungi wiki jana aliniomba maji niliyokuwa nakunywa kwenye chupa nikashangaa ila ikabidi nimpe, akauliza ninywe kidogo au nichukue yote nikasema chukua.
Nikasogea mbele nikashtuka, logic ya mtu kuniomba maji niliyokuwa nakunywa. Na mauzo siku mbili zilizofuata yalikuwa mabaya sana nikaona coincidence tu.

Ningefikiria vizuri ningempa hela akanunue mwenyewe
 
Yaani Hadi naogopa 😰😰.. sometimes hua najiuliza hivi Hawa hawana watoto maana sidhani kama Kuna mtu anapenda kumwona mzazi wake akiwa ombaomba
Wakati wewe mtoto unajiuliza na kumuonea huruma na yeye kama mzazi hataki kukuona unateseka kutembea ukiombaomba.Anaamua aende yeye mwenyewe. Upendo,huruma na kujali.
 
Kuna mbibi alivaa ushungi wiki jana aliniomba maji niliyokuwa nakunywa kwenye chupa nikashangaa ila ikabidi nimpe, akauliza ninywe kidogo au nichukue yote nikasema chukua.
Nikasogea mbele nikashtuka, logic ya mtu kuniomba maji niliyokuwa nakunywa. Na mauzo siku mbili zilizofuata yalikuwa mabaya sana nikaona coincidence tu.

Ningefikiria vizuri ningempa hela akanunue mwenyewe
Pole sana mkuu
 
Yaani Hadi naogopa 😰😰.. sometimes hua najiuliza hivi Hawa hawana watoto maana sidhani kama Kuna mtu anapenda kumwona mzazi wake akiwa ombaomba
Wengine unakuta watoto wamewapuuzia wazazi na wengine unakuta watoto na wao hawana mwelekeo wowote.
 
Back
Top Bottom