Wanaobeza ushindi wa Simba sc, wajue kuwa katika mechi 5 zilizopigwa mpaka leo hakuna timu iliyoshinda kwa tofauti ya zaidi ya goli moja

Wanaobeza ushindi wa Simba sc, wajue kuwa katika mechi 5 zilizopigwa mpaka leo hakuna timu iliyoshinda kwa tofauti ya zaidi ya goli moja

DullyJr

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
13,983
Reaction score
11,857
Nashangaa sana watu wanaobeza ushindi walioupata leo SIMBA SC, na ukichunguza kwa makini utagundua ni wivu na husda za kuona SIMBA wanazidi kuchanja mbuga.

Ukiangalia mpaka kufikia leo ktk mechi zote zilizochezwa za CAF CL na CAF CC hakuna hata timu moja iliyopata ushindi wa magoli zaidi ya mawili ,HAKUNA.

Timu zote zimepata ushindi wa tofauti ya goli moja tu....[emoji116][emoji116]angalia hapo chini. Hii ni tafsiri ya ugumu wa mashindano haya na timu zimejiandaa kwelikweli katika hatua hii kubwa.

Mimi naona tupunguze wivu haujengi,
Mchambuzi anaanza kuichambua game ya tarehe 24 na kusema tutapoteza kwa magoli mengi...dah

SIMBA HII ITAWAUMIZA KWELIKWELI,NA MTAKONDA NGEDERE NYIE.

Screenshot_2022-04-17-23-02-05-01.jpg
Screenshot_2022-04-17-23-02-49-92.jpg


Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
SIMBA 🇹🇿 NA AL MASRY 🇪🇬 pekee zimepata USHINDI KATIKA MECHI NNE ZA KOMBE LA SHIRIKISHO LA CAF.

FULL-TIME!

Martyrs of February Stadium, Tripoli
Al Ittihad SC 🇱🇾 0-0 🇱🇾 Al Ahli Tripoli

30 June Stadium, Cairo
Pyramids FC 🇪🇬 0-0 🇨🇩 TP Mazembe

Borg El Arab Stadium, Alexandria
Al Masry SC 🇪🇬 2-1 🇲🇦 RS Berkane
[Amr Marei, Haithem Ayouni || Hamza Regragui]
 
Habari za asubuhi wanajukwa

Nianze na kupongeza wanasimba kwa ujumla kwanzia wachezaji, management, na mashabiki wote wa simba na wapenzi wote wa soka kwa ushindi wajana

Nimeshangazwa na watu wanaobeza ushindi wa simba kisa tu idadi ya goli na wanaobeza ni wale waliotaka simba wafungwe mabao mengi zaidi au wapoteze kabisa.......watu hawafahamu kwamba hii ni robo fainali inaitaji uwe technical sana nimependa sana nidhamu ya simba jana .....ukitaka amini kwamba robo fainali ni ngumu angalia mechi zote za confederation tu kama kuna timu imeshinda kwa zaidi ya range ya magoli mawili .....
Screenshot_20220418-062006.jpg
 
Wewe timu Ina Mugalu na Kibu alafu unataka Magoli mengi uyatoe wapi!! Bila penalty ya mchongo na kuzima VAR ata ilo Moja halikuwepo.
 
Shida ni sisihatuwezi kucheza vizuri viwanja vya ugenini.. Ni ile timu ya gomez tu ndio tu ilipata droo na ushindi ugenini. Zile 4 kwa kaizer mpaka leo hata sielewi tulikufaje kufaje kwa wale walevi.
Ukitutoa sisi, wenzetu wana nidhamu kubwa mnoo ya ukabaji na game za away wanaweza kucheza, sisi huyu kocha hiyo game ya away ngoja akupangie kikosi hovyo, tunakufa 3 tunarudi kujipanga kwa game ijayo.


Laiti tukiweza kucheza kama mazembe jana, au tukaweza kukaba kama wao orlando basi hata huku kwenye mtoano tutakuwa tunapeta.
Binafsi matumaini ya kutoboa ni madogo mnoo, naweka 25%

Yote 9, hiyo game ya al masry bonge moja la mechi, yaani al masry kashinda 2-1 akiwa na red card 2.
 
Shida ni sisihatuwezi kucheza vizuri viwanja vya ugenini.. Ni ile timu ya gomez tu ndio tu ilipata droo na ushindi ugenini. Zile 4 kwa kaizer mpaka leo hata sielewi tulikufaje kufaje kwa wale walevi...
Kwa hiyo wewe uliwaona Orlando Pirates walikuja kwa Mkapa kupunguza idadi ya magoli tu?

Wewe unadhani timu ikiwa ugenini ni haki kufungwa, tena kufungwa magoli mengi?

Waza kwanza uwezo wa Orlando Pirates kabla ya mechi hii wakiwa ugenini, halafu tafakari uwezo wa Simba kwa jinsi walivyocheza jana.

Simba jana waliweza kucheza vizuri kuzuia kufungwa wakiwa uwanja wa nyumbani, wakacheza vizuri kuweza kupata goli la ushindi wakiwa nyumbani. Hayo ni matokeo na hatua njema ya kuweza kuanzia katika kujipanga game ya marudiano.
 
Punguza chuki wewe mwana Uto...

Mngefuzu nyie mfunge hayo magoli mengi
wanataka simba ishinde magoli mengi wakati wao walipigwa kagoli kamoja tu nyumban na ugenini.

Wao walishindwa kufunga hata hako ka goli kamoja kwenye uwanja wa nyumban,kuna wana uto wenye chuki zilizopitiliza na hawaufahamu mpira wanaongea ili kuleta mabishano yasiyo na msingi tu
 
Kwa hiyo wewe uliwaona Orlando Pirates walikuja kwa Mkapa kupunguza idadi ya magoli tu?
Wewe unadhani timu ikiwa ugenini ni haki kufungwa, tena kufungwa magoli mengi...
Unaweza ukasoma na usinielewe, hebu rudia tena kusoma mzee.
 
Kwa hiyo wewe uliwaona Orlando Pirates walikuja kwa Mkapa kupunguza idadi ya magoli tu?
Wewe unadhani timu ikiwa ugenini ni haki kufungwa, tena kufungwa magoli mengi...
Kwenye mpira wa miguu unapocheza away jambo la kwanza ni kuzuia kutofungwa kwa maana ya kutafuta sare, jambo la pili ni kutafuta goli la ugenini.

Na inapotokea imeshindikana na umeeuhusu goli basi jambo la tatu ni kufanya kila namna usifungwe magoli mengi ili ukawa na mlima mrefu kwenye mechi ya marudiano.

Alichoongea jamaa sidhani kama umemurlewa, hofu yake ni jinsi simba inavyocheza away msimu huu unampa mashaka ni heri wangepata advantage ya kuwapa Orlando mrefu wa kuupanda.

Mechi ya Simba vs Red arro, Simba walipata advantage ya magoli matatu lakini walivyoenda Zambia mpira waliocheza ulikuwa unasikitisha. Wale wazambia wangekuwa makini game walikuwa wanaimaliza first half, mechi ya berkane, ya Assec away.

Alichosema makaveli10 ni huko ugenini Simba wanabidi wabadilike ili kuweza kufuzu lasivyo watakutana na zahama
 
Unaweza ukasoma na usinielewe, hebu rudia tena kusoma mzee.
Mimi nilitaka kukupa tu hizi facts.
-Orlando wamekuwa wakivuna magoli wakiwa ugenini (Jana wameshindwa kuvuna goli ugenini)

-Kupata goli hata moja kwenye hatua hii ya robo fainali sio jambo rahisi sana. (Simba wamepata goli)

-Orlando Pirates iko juu kisoka kuliko Simba, kitendo cha Simba jana kuweza kuwamudu Orlando Pyrates kwa Mkapa ni mafanikio kwa Simba.
 
Nashangaa sana watu wanaobeza ushindi walioupata leo SIMBA SC, na ukichunguza kwa makini utagundua ni wivu na husda za kuona SIMBA wanazidi kuchanja mbuga...
Mkuu sijui point yako ni ipi ila kwa matokeo hayo ni kwamba hao wote waliokuwa away wanajua nidhamu ya kucheza away na ndio maana hakuna aliyefungwa 2+ inatakiwa Simba ifanyie mazoezi mbinu na ufundi za kucheza away ili wafanye kama hao walivyofanya away akatoe sare au akashinde au akaruhusu goli moja tu.
 
Kwenye mpira wa miguu unapocheza away jambo la kwanza ni kuzuia kutofungwa kwa maana ya kutafuta sare, jambo la pili ni kutafuta goli la ugenini. Na inapotokea imeshindikana na umeeuhusu goli basi jambo la tatu ni kufanya kila namna usifungwe magoli mengi ili ukawa na mlima mrefu kwenye mechi ya marudiano. Alichoongea jamaa sidhani kama umemurlewa, hofu yake ni jinsi simba inavyocheza away msimu huu unampa mashaka ni heri wangepata advantage ya kuwapa Orlando mrefu wa kuupanda.

Mechi ya Simba vs Red arro, Simba walipata advantage ya magoli matatu lakini walivyoenda Zambia mpira waliocheza ulikuwa unasikitisha. Wale wazambia wangekuwa makini game walikuwa wanaimaliza first half, mechi ya berkane, ya Assec away.

Alichosema makaveli10 ni huko ugenini Simba wanabidi wabadilike ili kuweza kufuzu lasivyo watakutana na zahama
Binafsi nimemuelewa, lakini nimetofautiana naye kimtazamo.
Msingi wangu ni kuwa, kabla ya kuwa underrate Simba kwa matokeo ya mechi ya jana alipaswa kwanza kutazama uhalisia. Na uhalisia ni kuwa Simba imeweza kupata ushindi nyumbani mbele ya timu ngumu ya Orlando Pirates. Huo ni mtaji kuelekea mechi ya ugenini.
 
Back
Top Bottom