Wanaochukia mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964 wana ajenda gani nyuma ya pazia?

Kuhusu Hanga siwezi kukuamini wewe pekee labda mzee Pandu Kificho kidogo naweza kumuamini!!!Lakini pia angekuepo Karume ili atudhibitishie zaidi
 
Historia ya zanzbar umetafiti kyanzia mwaka gani mzee wangu 1700,s au kuanzia mwaka 1964????
 
Historia ya zanzbar umetafiti kyanzia mwaka gani mzee wangu 1700,s au kuanzia mwaka 1964????
Nelson...
Nimesoma Ancient History.
Hii ni nyuma sana ya hapo.

Wakati mwingine hunyamaza kwa kukuonea huruma.
Nimehisi ulivyotaabika kusoma CV yangu.

Sikujisikia vizuri kukuonyesha kuwa ujiangalie.
Nisaidie ili tutunze heshima zetu.
 
Gavana...
Hawa hawana chochote kaka ni kibri tu.

Huyu kweli ndiye wa kunihoji mimi historia ya Karume?

Sheikh Mohammed hawa niliwashtukia
zamani hamna kitu hata kabla hajafungua hii thread nilimwona vile alivyokuwa akinijibu kuhusu kufa kwa ukristo West. Namwekea ushahidi anabisha tu . Haelewi makanisa yanauzwa na kununuliwa na waislamu na mengine yanageuzwa baa.
Tuwachukulie hivyo hivyo, na sidhani kama wanaweza kubadilika
Hivi wanavyoandika kuhusu Zanzibar inasikitisha eti hawa ni wasomi.
Haelewi huyo Karume huyo Bi Fatuma ni jamaa yetu. Kaka yake kaoa kwetu
Lile baraza la Mapinduzi la kwanza kuna mmoja ni Babu yangu halisi alimwoa Bibi ya gu mzaa Mama. Huyo Karume alikuwa mara nyingi haondoki nyumbani.
 
Mzee wangu sina tatizo binafsi na wewe

Nina tatizo kubwa sana na hoja zako dhalili

Tenganisha ninaposhambuliq hoja zako dhaifu na shambulio dhidi yako binafsi

Makala ulizoandika, vyuo ulivyohadhiri na mahusiano yako na wana mapinduzi yanaondoq credibility yako ikiwa unashindwa jibu maswali rahisi kama hali ya kisiasa na kijamii Zanzibar enzi za sultan

msomi kama wewe unaleta data za tafiti ya kificho ukidai ni za kweli? Like serious?

Mzee wangu sikutukani ila andika hoja zenye mashiko, jibu maswali kama unavyoulizwa mimi siishi kwenye wewe kuandika makala wala kufundisha vyuo vikuu mimi nadeal na specific issue ambayo hutaki kuijibu

Narudia sikutukani wewe as a person, nashambulia hoja zako

Kuhusu somo ninatamani sana kusoma lakini nitasomaje ilhali unaonesha una biasness

Hujibu maswali ya msingi, unaleta tafiti za kupikwa halafu unataraji nisome?
Nisome wakati hakuna material credible?

Siku ukija na tafiti credible niamini mzee nitajifunza kwako vinginevyo endelea na hao unaowaita wanafunzi wako

Nq Ikitokea nikaona kuna somo jingine unalimudu, hauko
Bias na una data credible niko tayari kujifunza ila kama utaendelea na hii trend ya kukwepa swali la msingi na kupika data jua nakuheshimu lakini sitaheshimu propaganda zako

Shikamoo yako mzee Saidi😂
 
Gavana...
Hawa hawana chochote kaka ni kibri tu.

Huyu kweli ndiye wa kunihoji mimi historia ya Karume?
Msomi yeyote haogopi kuhojiwa kwakuwa unadai unajua sisi hatukuamini eti kwakuwa uliwajua wanaMapinduzi hapana

Tunahoji mbinu zako za kitafiti na tunapata hitimisho kuwa tafiti yako ni credible na kama tutaendelea kukutana mzee wangu jua katu siwezi acha kukuhoji

Hoja ni lazima ili tuipate kweli

Kinahojiwa unachodai kukijua nothing personal

Sisi watu wa philosophy hii ndio kawaida yetu
 
Count...
Ahsante.
 
Gavana,
Hapo ndipo tunapoachana njia na hawa ndugu zetu.
 
Ahsante.
 
Gavana,
Nakuwekea picha ya moja ya misikiti iliyoko Cardiff, Wales.
Huu msikiti unaitwa ''Dar-ul- Isra.''

Huu ndiyo ulikuwa msikiti wangu.
Wahindi wa Pakistan walinunua kanisa wakaligeuza kuwa msikiti.

Wakanunua kanisa lingine jirani na hili lakini niliporudi Cardiff mwaka wa 1993 nikakuta bado liko vilevile hawajaligeuza kuwa mskikiti ila wanalitumia kama store ya kuwekea vitu.

 
Gavana,
Amani Thani ni mzee wangu.

Nilikutananae Dubai mwaka wa 1999 na akanipa kitabu chake, ''Ukweli ni Huu.''
Nakuwekea kitabu na saini yake katika kitabu hicho:


Aman Thani alinipa mswada wa kitabu chake kimoja nikafanyie uhariri.
Hii ilikkuwa mwaka wa 2016.

Kazi hii tuliifanya hadi ikakamilika ikabaki mimi kwenda Dubai tuupitie mswada ule kwa pamoja ili kitabu sasa kiende kwa ''publisher'' kichapwe.

Siku natoka nyumbani kwangu kwenda kukata tiketi nikapokea simu kuwa Mzee Aman Thani amepelekwa hospitali kalazwa.

Hazikupita hata siku mbili, tatu Mzee Aman Thani akafariki.

Hivi ndivyo kupitia watu kama hawa nilivyoweza kujifunza mengi sana katika historia ya Zanzibar.
 
Mashaallah
 
Mashaallah
Gavana,
Allah kanipendelea sana mimi.
Alhamdulilah.

SALA YA IJUMAA NILIKOPITA
Makala yangu ya Mfungo wa Ramadhani inaelekea imependwa na wengi.

Jamaa wamenifata pembeni kutaka kunijua zaidi.

Jambo hili limenifanya nifikirie makala nyingine yenye mwelekeo huo huo.

Nitarejea In Shaa Allah lakini nakuacha na picha ya Msikiti wa Geneva na Msikiti wa Humburg ambako nilisali sala ya Ijumaa mwaka wa 2011.

Huu msikiti wa Humburg unaitwa Masjid Al Nour sawa na jina la msikiti wa mtaani kwangu Magomeni Mapipa.

Nimeupenda msikiti huu kwa hili jina.

Sala yangu ya kwanza ya Ijumaa kusali nje ya Tanzania nilisali msikiti wa Montaza Palace, Alexandria, Misri mwaka wa 1988.

Huu msikiti ni mzuri wa sifa.

Montaza Palace wakati wa Mfalme Farouk ilikuwa kasri ya mfalme akija kupumzika wakati wa kiangazi.

Msikiti huu ukajengwa katika makazi ya Mfalme Farouk.

Baada ya mapinduzi ya mwaka 1952 Montaza Palace ikiwa nyumba ya wananchi wa Misri.

Niliijua nyumba hii miaka mingi nyuma nilipoisoma kwenye kitabu cha Mohamed Heykal, "The Road to Ramadan," kitabu alichoandika kuhusu Vita Vya Yom Kippur vya 1973 kati ya Misri na Israel.

Katika kitabu hicho kuna sehemu Heykal anaeleza vituko vya Anwar Sadat alipomfuata kutoka Cairo kuja Montaza Palace Alexandria kupata kauli yake jinsi vita vilivyokuwa vinaendelea.

Nilipokwenda Cairo nikasali Ijumaa msikiti mmoja uko katikati ya mji jirani ni ilipo Egyptian Museum.

Ninachokumbuka msikiti huu ni kuwa sikuweza kuingia ndani msikitini kwa kuwa msikiti umejaa hadi nje watu wengi wako wengi nje barabarani.

Sifa kubwa ya mji wa Cairo ni wingi wa watu na wingi wa magari barabarani Waingereza wanaita, "bumper to bumper," na madereva wanashindana kupiga honi.

Mwaka uliofuatia nikaenda Sudan nikasali Sala ya Ijumaa msikiti wa Chuo Kikuu Cha Khartoum mwaka wa 1989.

Nilifika Sudan miezi michache baada ya Omar Bashir kupindua serikali na kutwaa madaraka.

Picha iko hapo chini utaitambua kwa kanzu na vilemba vya Kisudani.

Mwaka wa 1991 nimesali msikiti mkuu wa Glasgow, Scotland.

Katika misikiti niliyopata kusali sijapata kusali msikiti nikawa mimi ndiyo mtu mweusi peke yangu ndani ya msikiti kiasi watu wote ndani ya msikiti wananishangaa.

Naingia msikiti macho yote yako kwangu.

Nasali, ''tahiyatu masjid,'' yaani sala ya kuuamkia msikiti, macho yote ndani ya msikiti yako kwangu.

Jambo hili lilinifanya nijisikie vibaya.

Baada ya sala nimeingia kwenye duka la vitabu la msikiti.

Ndugu zangu Waislam wakanifuata kunisalimia na wakawa wananiuliza maswali.
Walitaka kujua wapi natoka na lini nimeingia Uislam?

Hawajui kuwa mimi ni mjukuu wa Sheikh Muhammad Mvamila.
Hawa ndugu zangu hawaijui Tanzania wala hawajapata kuisikia.

Nilipowaeleza kuwa nimezaliwa Muislam wakataka kujua Uislam umeingia lini Tanzania.

Walishangaa sana nilipowaeleza kuwa Uislam upo kwetu miaka 1000.

Nimesali Ijumaa Edinburgh.

Nilikwenda Edinburgh kwanza kuona Edinburgh Castle na kukitembelea chuo alichosoma Mwalimu Nyerere.

Edinburgh Castle ni sehemu inatembelewa sana na watalii na ni majumba mengi kwenye mlima mkubwa.

Hii mijumba ya kale iko hapo karne kwa karne.

Sehemu hii ilinikumbusha Macbeth wa William Shakespeare.

Niliyoshuhudia msikiti wa Glasgow sikuyaona Edinburgh hapo niliwakuta watu weusi wengi wao wakiwa wanafunzi kutoka Afrika.

Nimesali Ijumaa Msikiti wa Makka na Madina mwaka wa 1997, 1998 na 2014.

Mwaka wa 1997 nilikwena Umra na 1998 na 2014 nilikwenda hijja.

Hijja ya 2014 nilipata mwaliko kutoka kwa Mfalme wa Saudia.
Waalikwa tulikuwa wengi kutoka Tanzania na kwengine ulimwenguni.

Picha hiyo hapo chini nimeupiga Masjid Badawy, Msikiti wa Mtume SAW kutoka dirisha la chumba cha hoteli niliyofikia 2014.

Nilinunua camera si mbali na Msikiti wa Mtume na nikajiambia kuwa picha yangu ya kwanza kupiga uwe Msikiti wa Mtume.

Hili nikalifanya.

Nimesali Ijumaa Tehran pamoja na Rais wa Iran Ahmed Najad mwaka wa 2007.

Nimesali Ijumaa Grande Mosque, yaani Msikiti Mkuu, Paris 2011.
Huu nidyo msikiti mkubwa Paris na Imam Mkuu ni Mngazija.

Hiyo picha hapo chini nimepiga na jamaa wa Kingazija nje ya msikiti.

Kulia kwenye picha ni rafiki yangu marehemu Salim Himid.

Nimesali Ijumaa New York mwaka wa 2011 kwenye kijimsikiti kidogo Manhattan, New York.

Msikiti huu nilikuta jamaa ndogo katika Sala ya Ijumaa si kama jamii nilizopata kuona kwengineko duniani.

Nje ya msikiti kuna askari wanafanya doria kulinda msikiti na wanaosali hapo.

Nimesali Ijumaa Istanbul mwaka wa 2015.

Takriban msikiti mzima watu wamepiga suti.

Sijui kama ni kawaida kuvaa suti au kwa sababu ulikuwa wakati wa baridi.

Nimesali Ijumaa Dubai Rashidiyya mwaka wa 2016.

Hii ni sehemu ambayo Wazanzibar waliotafuta hifadhi Dubai baada ya mapinduzi walipewa makazi hapo na kujengewa nyumba na Sheikh Rashid.

Sala ya Ijumaa Msikiti wa Rashidiyya utasema uko Masjid Jibril Zanzibar.



 

Mashaallah, Shukrani sana

Tumefaidika sana , Allah akupe kheri nyingi, duniani na Akhera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…