Wanaodaiwa kumuua Dk. Mvungi watinga kortini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Wakiwa mahakamani tayari kabisa kupandisha kizimbani na kusomewa kesi yao.


Watu kumi akiwamo mlinzi wa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, marehemu Dk. Edmund Mvungi, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kumuua kwa makusudi.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
Wakili wa Serikali, Aida Kisuma, alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo, kuwa washtakiwa hao ni Chibago Magozi (32), mkazi Vingunguti, John Mayunga (56), mkazi wa Kiwalani, Juma Kangungu (29), mkazi wa Vingunguti, Longishu Losingo (29), mlinzi, mkazi wa Kariakoo Msimbazi.

Wengine ni Masunga Msukuma (40), dereva, mkazi wa Kitunda, Paulo Mdonondo (30), mkazi wa Tabata, Mianda Mlewa (40), mkazi wa Vingunguti, Zacharia Msese (33), mkazi wa Buguruni, Msigwa Matonya (30), fundi Mwashi mkazi wa Vingunguti na Ahmad Kitabu (30), mkazi wa Kinondoni Mwananyamala.

Wakili Kisuma alidai mahakamani hapo kuwa, washtakiwa wanakabiliwa na shtaka la kuua kwa kukusudia.

Alidai kuwa Novemba 3, mwaka huu, eneo la Msakuzi Kiswegere, washtakiwa hao kwa pamoja walimuua Dk. Edmund Mvungi kwa kukusudia.
Wakili Kisuma, alidai upelelelezi wa shauri hilo bado unaendelea na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa kesi inayowakabili inasikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kesi hiyo itakuja tena kwaajili ya kutajwa Disemba 5, mwaka huu.
Washtakiwa hao walifikishwa katika eneo hilo la mahakama chini ya ulinzi mkali wa polisi waliokuwa na silaha za moto.

Washtakiwa hao waliondoka mahakamani wakiwa ndani ya gari la polisi namba Kxo6 EFD na kusindikizwa na gari aina ya Noah namba T539 CCB likiwa na askari wenye silaha za
moto.

Alisikika mtuhumiwa mmoja akimlaumu mwenzie kuwa alimpigia simu, kumbe simu aliyokuwa anaitumia ni ya wizi, na pia alimtuhumu mwenzie kuwa ni jambazi.

Awali, Dk.Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya
Chama cha NCCR-Mageuzi alifariki dunia akiwa nchini Afrika Kusini ambako alipelekwa kwa matibabu baada ya kushambuliwa Novemba 3, mwaka huu, nyumbani kwake.



CHANZO: NIPASHE

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…