Wanaodhaniwa panya road waibukia Dodoma watu watatu wajeruhiwa

Wanaodhaniwa panya road waibukia Dodoma watu watatu wajeruhiwa

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Watu watatu wamejeruhiwa kwa kukatwa na mapanga na kikundi cha watoto wahalifu wenye umri chini ya miaka 18 katika Mtaa wa Msangalalee Magharibi, Kata ya Dodoma Makulu, jijini Dodoma. Vitendo hivyo vimetokea baada ya watu hao kukataa kutoa fedha walizoombwa na watoto hao.

Matukio hayo yaliripotiwa kutokea kwa siku tatu mfululizo, kuanzia Desemba 12 hadi 14, 2024, kati ya saa 2:00 na saa 3:30 usiku, huku waathirika wakivamiwa wakati wakirejea majumbani baada ya shughuli za mchana kutwa.
Wakizungumza na vyombo vya habarl leo Jumapili, Desemba 22, 2024, baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema kuibuka kwa kundi hili la watoto wahalifu kumeongeza hofu miongoni mwao, hasa nyakati za usiku.

“Tunaishi kwa hofu sasa. Unapita usiku unajiuliza kama utavamiwa au la,” amesema mmoja wa wakazi wa mtaa huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma George Katabazi amesema jeshi hilo limekuwa likifanya doria za mara kwa mara kwenye mitaa yote ya jiji la Dodoma ili kudhibiti vitendo vya uhalifu ambavyo vimekuwa vikifanywa na makundi ya wahalifu ambapo kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kuyadhibiti makundi hayo

Chanzo: Kahama Fm

Snapinsta.app_471410958_1421609842137081_8567242760413134549_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom