Wanaofahamu Kiswahili cha Kenya, naombeni msaada wenu hapa

Ni ugawanyaji wa madaraka kuelekea ngazi za chini za uongozi, yaani ni kuzipa Serikali za majimbo au za mitaa mamlaka makubwa zaidi.
 
Sio Kenya tu.. Hata. Tanzania ... Ugatuzi ni istilahi yenye maana ya Ugawanywaji wa madaraka kutoka juu kwenye Ngazi ya maamuzi (serikali kuu) na kuileta chini kwenye Ngazi za serikali za mitaa (mahsusi Halmashaur, tarafa, kata na hata vijiji/mtaa)
 
Binafsi Wakenya kuna baadhi ya maneno ya kiswahili nawakubali, mfano shule ya "upili" badala ya shule ya "sekondari"
 
Ipo tofauti kati ya devolution na decentralization? Tatizo ni kuwa maneno mengi ya Kiswahili yanabuniwa na watu wachache badala ya kubuniwa na jamii la kiswahili. Viongozi wetu hutukosea sana kwa kukosa maono.

Kwa mfano, Neno Stakeholders lilikuwa likijulikana kama Washika Dau. Siku hizi, ni wadau. Kwani nini kilifanyika?
 
neno wadau. lilifanyiwa uhulutishaji njia mojawapo ya kuunda maneno ya lugha ya kiswahili yenye maana ya kuchukua sehemu ya neno na kuunda neno lingine .washika dau ilichukuliwa neno wa na dau tukapata wadau lengo ikiwa ni kurahisisha utamkaji wake
 
Back
Top Bottom