Wanaofanya biashara mitandaoni watakiwa kujisajili TRA

Wanaofanya biashara mitandaoni watakiwa kujisajili TRA

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Baadaya ya manyunyu kutamaradi, sasa mvua inaweza kunya wakati wowote.

"Watu wote wanaofanya biashara kidigitali tunawaomba mfike katika ofisi zetu kwa ajili ya usajili wa biashara hizo"

"Sambamba na hilo tunaendelea kufatilia wateja wenu mnaowahudumia ili tupate taarifa sahihi za biashara zenu"

"Tunatambua kuna watu hawana maduka na hawana TIN kwa ajili ya biashara wanazofanya"

"Na wengine wana maghala makubwa ya kuhifadhi bidhaa na kisha kuuza kidigitali. Sasa nyinyi nyote mnapaswa kuja kujisajili".
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wanaofanya biashara kidigitali wafike ofisini na kujisajili kwa kufanya biashara hizo.

TRA wamesema wanatambua kuwa kuna watu hawana maduka na Namba ya Mlipa Kodi (TIN) japo wana maghala makubwa ya kuhifadhia bidhaa na huuza kidigitali.

TRA wanaendelea kufatilia wateja wa biashara za kidigitali ili tupate taarifa sahihi za biashara hizo.
Screenshot 2022-03-11 at 12-48-01 TRA Tanzania (@TRATanzania) _ Twitter.png
 
Baadaya ya manyunyu kutamaradi, sasa mvua inaweza kunya wakati wowote.

"Watu wote wanaofanya biashara kidigitali tunawaomba mfike katika ofisi zetu kwa ajili ya usajili wa biashara hizo"

"Sambamba na hilo tunaendelea kufatilia wateja wenu mnaowahudumia ili tupate taarifa sahihi za biashara zenu"

"Tunatambua kuna watu hawana maduka na hawana TIN kwa ajili ya biashara wanazofanya"

"Na wengine wana maghala makubwa ya kuhifadhi bidhaa na kisha kuuza kidigitali. Sasa nyinyi nyote mnapaswa kuja kujisajili".
Sawa,,,,,tunaomba pia report za mapato na matumizi.
 
Wafuateni kwenye maghala siyo kutuchafulia hali ya hewa humu.

Mtu anauza dagaa tu tayari mnataka awafuate mmtongoze
 
Tatizo kubwa la "watanzania wanyonge" wanaona tu matajiri ndio wanatakiwa kulipa kodi. Wao haiwahusu kabisa. Mi naona hata muuza pipi angelipa kodi hata kama ni Tshs.20/-
 
Sahivi kuna mtindo "mmachinga" anapaki Canter/kirukuu pembeni ya barabara na imejaa bidhaa za duka zima. Anauza na kusepa bila kulipia chochote.
 
Wengine tayari wana tin, leseni na maduka, ila kwa ugumu wa biashara amejiongeza na kuuzia mtandaoni, sasa huyu naye vipi
 
Wengine tayari wana tin, leseni na maduka, ila kwa ugumu wa biashara amejiongeza na kuuzia mtandaoni, sasa huyu naye vipi
Sasa umeshasema ana leseni, maana yake ameshajisajili, au unataka na KFC na Pizzahut wanaouza vyakula mtandaoni wakajisajili tena?
 
Back
Top Bottom