Wanaogopa nini kuandamana?

Wanaogopa nini kuandamana?

Iyegu

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
6,276
Reaction score
12,404
"Maandamano ya kupinga ada ya vyuo vikuu Afrika Kusini"
Wiki iliyopita, wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Afrika Kusini walianza kufanya maandamano ya kupinga ongezeko la ada kwa asilimia 10.5 katika muhula wa 2015-2016.

Uamuzi huo uliamsha hisia tofauti miongoni mwa wanafunzi walioamua kufunga milango ya vyuo vikuu na kusitisha masomo.

Waziri wa Elimu nchini Afrika Kusini Blade Nzimande, ametoa wito kwa utawala wa vyuo vikuu kujadili tena suala la ada na kuchukuwa uamuzi sahihi ili kurudisha hali ya kawaida vyuoni.

Akizungumza na vyombo vya habari, Nzimande alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha wanafunzi wasiokuwa na uwezo wanapata haki yao ya elimu.

Nzimande aliongezea kusema kuwa uamuzi huo wa kuongeza ada utaathiri wanafunzi wanaotoka kwenye familia fukara na hivyo basi, utawala wa vyuo vikuu unapaswa kujadili suala hilo na wanafunzi.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

"Maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu Chile"

Maelfu ya wanafunzi walifanya maandamano mjini Santiago kupinga mabadiliko ya mfumo wa elimu yanayopangwa kuletwa na serikali.

Takriban wanafunzi 80,000 walikuwa wakiishutumu serikali ya Chile kwa kutaka kupandisha ada za vyuo vikuu.

Polisi walilazimika kutumia vitoa machozi na maji moto kukabiliana na wanafunzi hao waliokuwa wakiwarushia mawe.

Hapo jana, serikali ya Chile iliwahi kutangaza mpango wake wa kupandisha ada za vyuo vikuu katika mwaka wa 2016.

Mabadiliko ya mfumo wa elimu yaliyopendekezwa yanatarajiwa kuwasilishwa bungeni mwezi Desemba. Hivyo basi, wakuu wa taasisi za elimu wanapaswa kujadili mapendekezo hayo kabla ya mwezi Desemba.
>>>>>>>>>>>

Jumanne, 20 Mei 2014
WANAFUNZI CHUO CHA NAIROBI WAANDAMANA KUPINGA ONGEZEKO LA ADA.

Wanafunzi walitawanywa kwa kutumia gesi ya kutoa machozi
Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Kenya wamezua vurugu wakipinga mpango wa serikali kutaka kuongeza karo katika vyuo vikuu vyote vya umma.

Polisi walipambana na wanafunzi hao kwa kutumia gesi ya kutoa machozi kutawanya wanafunzi hao ambao walizua vurugu mjini na kuwapora abiria huku wakiharibu magari ya umma na yale ya abiria katika barabara kuu ya Uhuru katikakati ya jiji la Nairobi.

Pia waliripotiwa kuvunja maduka na kuharibu mali ya watu.
Wachuuzi walilazimika kuondoka mjini huku polisi wakipambana na wanafunzi hao ambao waliungana kutoka vyuo vikuu mbali mbali kote nchini Kenya.

Awali maandamano yao yalikuwa salama ingawa baadaye wanafunzi hao walioanza kuandamana tangu saa nne asubuhi walianza kuzua rabsha na kulazimisha polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya.

Wanafunzi hao wanaandamana kupinga mapendekezo ya serikali kuongeza karo ya vyo vikuu , ingawa waziri wa elimu ya juu Profesa Jacob Kaimenyi amesema kuwa serikali bado haijatoa tamko rasmi ikiwa wanafunzi wa vyuo vikuu watalazimika kuongeza karo.

Alisema kuwa ripoti kuwa karo itaongezwa sio sawa na ni za kupotosha akisisitiza kuwa ikiwa jambo kama hilo litafanyika litahitajika kutangazwa na baraza la vyuo vikuu nchini humo baada ya makubaliano kufikiwa.

Wanafunzi hao wanapinga mpango wa serikali wakisema kuwa kuambatana na mfumuko wa bei, karo yao haipaswi kuongezwa na kwamba serikali inapaswa kushauriana nao kabla ya kufikia hatua zozote za kuongeza karo.
Wanafunzi watano wameripotiwa kujeruhiwa katika vurugu hizo.

BBC.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Wanafunzi wa chuo waandamana DR Congo




    • 16 Novemba 2015
      Wanafunzi wa chuo kikuu kimoja nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo leo wameandamana Kinshasa kulalamikia kuongezwa kwa ada ya masomo.

      Wanafunzi hao kutoka taasisi ya taifa ya uhandisi wamefunga barabara na kuchoma magari matatu karibu na bewa la chuo kikuu hicho.
      Polisi wamewakamata waandamanaji 10, anaripoti.

      Ada ya masomo imeongezeka kutoka takriban $300 (£200) hadi $500.
    • ********
 
Hapa kwetu masharobalo ni wengi kuliko radicals,alafu hakuna umoja wa kweli kwa wanafunzi wa kisasa bali mapenzi yameshika hatamu.
 
Back
Top Bottom