KERO Wanaohusika kudai fedha za ‘parking’ kwa kusimamisha magari barabarani, wamekuwa kero kwa Wananchi!

KERO Wanaohusika kudai fedha za ‘parking’ kwa kusimamisha magari barabarani, wamekuwa kero kwa Wananchi!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakusanya malipo ya maegesho (parking), kwa kuvamia kando ya barabara na kuanza kukusanya malipo wamekuwa kero sana na mara nyingi wamekuwa wakiona ufahari kusumbua wenye magari.

Hii hali ina kera sana kupoteza muda wa Wananchi. Wananchi kweli anapaswa hulipia lakini kwanini wasiweke njia nzuri ya kukusanya fedha hizi? Matokeo yake anafanya masuala bila utaratibu na kwa njia za ovyo kabisa.

Kuna hawa watu sijui ni kutoka TARURA au Halmashauri, wamekuwa kero kubwa, hawa wanachokifanya ni kutafuta sehemu yoyote ya barabara na kujipanga kwa wingi.

Ukipita wanakusimamisha na wanakuja wengi kwenye gari lako na kuanza kukuhoji huku wakionesha deni unalodaiwa kwenye maegesho ya magari.

Hutaratibu ni kwa kipuuzi na ovyo kabisa, ni kama wanakusonga ili wakutapeli usipate muda wa kuangalia kweli unachodaiwa.

Hadi naandika hivi kwa mara zaidi ya 3 nimekutana na hawa watu, jana walijipanga barabara ya Bagamoyo ya zamani, kwenye kituo cha karibu na Makao Makuu ya JKT, JKT Bus Stand.

Kwanza walisababisha foleni isiyo ya lazima kabisa, pili sijui wapo chini ya nani na wanafundishwa na nani kwamba kuvamia mtu kwa kundi ndio njia nzuri ya kudai maegesho ya gari.

Walinambia kuna hela nadaiwa na nikailipa kuondokana na kero ya kusongwa na kusemeshwa na watu zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.

Kama utaratibu huu unatumika kwanini tunalipa kwa mtandao parking kutumia Application ya TARURA? Naelewa labda kuna wasiolipa, kwanini utaratibu mzuri usitumike kuliko huu wa kuvamia watu kama majambazi?

Wanaohusika na hawa watu tafadhali angalieni njia nzuri huu upuuzi mnaofanya sio wa kiungwana kabisa.

JIREKEBISHENI

Maegesho 1.jpg

Maegesho 2.jpg

Maegesho 3.jpg

 
Halafu namba Yao ya kuangalia deni haifanyi kazi. Huu nao ni uzembe mwingine
 
Wanakimbizana na mwaka wa fedha. wa Serikali unaoisha June 31 ,2024...yote kwa yote ni WAPUUZI
 
Walinambia kuna hela nadaiwa na nikailipa kuondokana na kero ya kusongwa na kusemeshwa na watu zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja
Tatizo lipo kwenye kulimbikiza pesa na kuzilipa ili kuondokana na kero ya kusongwa na kusemeshwa na watu zaidi ya mmoja.
 
Back
Top Bottom