Wanaoishi maghorofani hawajali wanaoishi chini?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Sijui ni kukosa utu, kujali, au kukosa maadili! Inakuwaje watuwengine wanaishi maghorofani ni kana kwamba hawajali wanaoishi chini. Kwani ni lazima iwe ugomvi. Maana angalau nyumba zinazopakana chumba usumbufu unaweza kuwa ni kelele zaidi lakini wanaoishi ghorofani wakati mwingine utafikiria wanagombana na kuta, vitanda, milango na sakafu!

Sijui watu wengine wakoje! ngoja na miye ni bibi yenu tuhamie maghorofani!

Issh!!!
 
Maadili mabovu ndo source!
 
Mkuu upo floor ya chini nini? mbona unalalamika sana? kama anagonga sakafu na wewe simgongee dari la zege apate utamu wake?
 
Mkuu upo floor ya chini nini? mbona unalalamika sana? kama anagonga sakafu na wewe simgongee dari la zege apate utamu wake?

aisee sijui hawa vijana ndio wametoka fungate maana wameniharibia siku yangu kabisa; next time sigongi floor nawagongea kengele yao hapo nje. Utadhani wako kwenye Olimpiki ya Chumbani!

Issssh!
 
aisee sijui hawa vijana ndio wametoka fungate maana wameniharibia siku yangu kabisa; next time sigongi floor nawagongea kengele yao hapo nje. Utadhani wako kwenye Olimpiki ya Chumbani!

Issssh!

Pole mkuu, ngoja niwe mtabiri kama shekhe Yahya hao wametokea huku Kwetu Africa ndio wenye tabia za kugonga floor bila ya kujali watu waliochini,tena west
 
Aache kujipa staarehe kisa Mwanakijiji yupo chini?
 
Imebidi niwagongee leo asubuhi unajua jibu lao lilikuwaje guess...
 
Hayo mambo yalinifanya nigombane na jirani yangu . Ana pounds kama 270, akitembea tu nasikia mihatua yake, siku akaja na bwana wake kjama 300 pounds...picha za ukutani zikaanza kudondoka. Solution ni kugonga dari lako mpaka kieleweeke.
 
dawa yao ndogo hao!chukua bangi halafu ulipulize ile mbaya,moshi wote utaelekea juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…