Wanaojiandaa kufunga starlink Internet ya Elon Musk wakidhani ni bei chee wanaota ndoto za alinacha,

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Nashangaa sana kuona watu wanayopotoshana kwamba ujio wa starlink Internet hapa Tanzania ndio utakuwa suluhisho la unlimited internet ghali kama supakasi ya voda.

Kama hauwezi kumudu internet unlimited ya supakasi kwa 115,000 basi ondoa shaka kabisa kwamba star link itabaki kuwa ndoto daima.

Unawaza unafuu wa bei (afordability) ?

Dola $ 99 kila mwezi ? dola moja hio ni 2,300, zidisha upate majibu. hio bili utaweza kuimudu kila mwezi ?

Kufungiwa hio huduma hata tukionewa huruma tupo Africa haiwezi pungua chini ya milioni, utaweza ?

Faida ya starlink ni kwamba itapatikana miji na majiji karibu yote, vijiji karibu vyote, wilaya karibu zote, maporini, n.k tofauti na supakasi ambao katika kila mkoa ukiachana na Dar huwa wapo kwenye wilaya moja kuu tu. tena ni maeneo ya centre.
 
Nisaidie...

GB1 ni USD ngapi huko U.S.A..?

Hapa Kwa Samia ni Kuanzia Tsh 2000 - 2500 ( $ 1)

Tuanzie hapo kwanza...
 
Starlink ni internet ya Majumbani fixed, haipimwi kwa GB.

Hata Tanzania Internet za Majumbani ama maofisini hazipimwi kwa GB.
 
Kama Tshs. 30,000 unapewa GB 19 trna ambazo kwa wengine matumizi yetu wiki sitoboi. Kwa mwezi ni Tsh. 120,000 kwanini nisitumie starlink tena unlimited.
 
120k ni vodacom supakasi, starlink sasa hivi ni $110~ shilingi 256,520.00 huduma ya setilaiti intaneti ya bei nafuu kama ingekuwepo TZ ni ViaSat ambayo inapatikana Kwa $30@12mbps ambayo bado ni gharama kuliko ttcl fiber au zuku
 
Nashangaa sana kuona watu wanayopotoshana kwamba ujio wa starlink Internet hapa Tanzania ndio utakuwa suluhisho la unlimited internet ghali kama supakasi ya voda.

Kama hauwezi kumudu internet unlimited ya supakasi kwa 115,000 basi ondoa shaka kabisa kwamba star link itabaki kuwa ndoto daima.

Unawaza unafuu wa bei (afordability) ?

Dola $ 99 kila mwezi ? dola moja hio ni 2,300, zidisha upate majibu. hio bili utaweza kuimudu kila mwezi ?

Kufungiwa hio huduma hata tukionewa huruma tupo Africa haiwezi pungua chini ya milioni, utaweza ?

Faida ya starlink ni kwamba itapatikana miji na majiji karibu yote, vijiji karibu vyote, wilaya karibu zote, maporini, n.k tofauti na supakasi ambao katika kila mkoa ukiachana na Dar huwa wapo kwenye wilaya moja kuu tu. tena ni maeneo ya centre.
Bro hivi vitu si vya kila mtu. Starlink haiji kuokoa watu wasioweza access internet kwa bei nafuu. Starlink inaongeza chaguo na ushindani. Starlink is not for everyone.
 
Back
Top Bottom