Wanaojiita 'Jr' wanamaanisha nini?

Esayi

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2017
Posts
355
Reaction score
146
Mimi napenda leo kuuliza sijui kabisa.

Wana JF huko Facebook naonaga watu wanajiita...Tz nawaelewa maana yao.

Lakini sasa je hawa wakina Jr ii, Jr iii, Jr, ndo wanamaanisha nini?

Ahsante wakuu JF
 
naomba kuuliza pia
kwa mwanaume huwa wanaitwa Sir
kwa wanawake wanaitwa Madame

ni kigezo kipi sasa hutumika kumuita mtu mmojammoja Sir?

kwa mfano tuna Sir alex furgerson, wala hutasikia tukiita Sir Zinedine zidane
wakati hiohuo tunae sir Isaack newton lakini hatuna Sir Apollo
 
Mimi napenda leo kuuliza sijui kabisa.

Wana JF huko Facebook naonaga watu wanajiita...Tz nawaelewa maana yao.

Lakini sasa je hawa wakina Jr ii, Jr iii, Jr, ndo wanamaanisha nini?

Ahsante wakuu JF
Hizo Jr II, au Jr III, inamaanisha ni Jr wa pili au wa tatu katika ukoo wenu.

Kwa mfano, unaweza ukapata mtoto wa kiume, ukampa jina lako Elias McDonald.
Kwa kuwa wewe ni mkubwa automatically utakuwa Elias McDonald Sr (Senior) na mwanao atakua Elias McDonald Jr.

Mwanao akipata mtoto wa kiume akampa jina hilo hilo, jina litakua Elias McDonald III (Elias McDonald the third) au Elias McDonald wa tatu. Akishaingia mtu wa tatu kwenye mfululizo wa jina moja kwenye ukoo, zile senior na junior zinapotea, senior atakuwa 1st, junior atakua 2nd na wa tatu atakua 3rd and so on.

Elias McDonald I
Elias McDonald II
Elias McDonald III
.
.

Senior na Junior zitakwepo kama wenye jina hilo ni wawili tu katika ukoo wenu.
 
Ahsante lakin naona sasa mtu na mdogo wake ni majunior
Hiyo ya mtu na mdogo wake Siielewi. Ila kwa kawaida kama baba mzazi anaitwa Juma Kilo na amezaa mtoto akiamua kumwita jina hilohilo, basi atakuwa Juma Kilo Jr.
 
Jr ni dabo humo kwa majina mawili, ila ujue babu yako pande zote 2 na uwe kidume wa kwanZa kupewa u bin utapewa hiyo heshima.
 
Kwahiyo ili awe jr lazma awe uzao wangu???
Je kama ndugu, mfano mtoto wa ba mkubwa anaitwa Evelyn na mie wa ba mdogo Evelyn.... Mie siwezi kuwa Evelyn jr? Na pia Jr inatumiwa na jinsia zote?
 
Kuiga tu ni kama tulivyoiga majina ya kizungu kama John, Charles etc
 
ni kikundi cha waganga na wachawi wa siri waliopo Jf ambao hutumia muda mwingi ktk shughuli za kuwanga na kuagua.
wanafanya mambo yao kwa siri sana ila wanae mwanachama wao mmoja ambae ni mpare.
huyu jamaa anaitwa jina mshana jr kama sikosi ye ni msaliti anaetoa siri zao.
"natania"
 
Ninga sikutegemea kuona commen ya aina hii kutoka kwako. Watu wengi wanauliza humu ili kuchota maarifa. Kama vipi mkuu si upite kimya? Usisheshe hadhi ya GT kiasi hicho mkuu, yapo majukwaa ya utani, hayo ndio yanastahili comments za aina hiyo.

Vv
 
Ukimuona mtu anajiita Jr ujue anatumia jina la ubin la baba yake, mfano alibakari jr, siku ukikuta jina hilo elewa huyo atakuwa ni mwanangu muda huo mimi nitakuwa najulikana kama alibakari sr.
Mwanangu anaweza kujiita kwa jina langu lakini neno jr linamaanisha mdogo, wakati mimi nikijiita alibakari sr namaanisha mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…