DOKEZO Wanaokatisha tiketi za kieletroniki waangaliwe

DOKEZO Wanaokatisha tiketi za kieletroniki waangaliwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mchaga Tajiri

Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
10
Reaction score
16
Kumeibuka tabia ya baadhi ya wakatisha tiketi za kieletroniki kwa mabasi yaendayo mikoani kupokea pesa tofauti na ile inayokatwa kwenye tiketi.

Kulingana na bei ya nauli za mabasi yaendayo mikoani iliyotolewa na SUMATRA mwezi Januari 2023 inaonesha kuwa kutoka Dodoma hadi mkoani Morogoro nauli ni shilingi 16,700.

Ukipanda magari hayo hadi Morogoro wanakuchaji kiasi cha shilingi 20,000 huku kwenye tiketi ikiandikwa kiasi cha shilingi 18,000.

Nikiwa mmoja wa watu waliokutana na changamoto hii nilibaini hilo baada ya kukagua tiketi yangu nilipo fika Morogoro.
 
Back
Top Bottom